MNEC HAMOUD JUMAA AMTAJA SILVESTRY KOKA KUWA MBUNGE HODARI WA UTEKELEZAJI ILANI YA CCM



Na Gustaphu Haule, Pwani 

MJUMBE wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi ( CCM) Taifa ( MNEC) Hamoud Jumaa amemtaja Mbunge wa Jimbo la Kibaha Mjini Silvestry Koka kuwa ni mmoja kati ya wabunge vinara na hodari waliotekeleza vizuri ilani ya CCM katika majimbo yao.

Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa Hamoud Jumaa (MNEC) katikati mwenye shati la njano akiwa pamoja na Mbunge wa Jimbo la Kibaha Mjini Silvestry Koka na Kulia kwake ni mwenyekiti wa CCM Kibaha Mjini Mwajuma Nyamka katika mkutano Mkuu maalum wa Jimbo la Kibaha Mjini uliofanyika Aprili 26,2025.

Jumaa, amesema ametembea katika majimbo mengi hapa nchini lakini akijaribu kufananisha anaona Jimbo la Kibaha Mjini kuna kazi kubwa imefanyika na maendeleo zaidi yanaonekana kupitia Koka.

Jumaa, ametoa kauli hiyo Aprili 26, 2025 wakati akizungumza na wajumbe wa mkutano mkuu maalum wa Jimbo la Kibaha Mjini ukiwa ni sehemu ya  kuwasilisha taarifa ya utekelezaji wa ilani ya CCM katika kipindi cha mwaka 2020/2025 chini ya mbunge Koka.

Jumaa ambaye alikuwa mgeni rasmi katika mkutano huo amewaambia wajumbe hao kuwa Kibaha Mjini ilani imetekelezwa vizuri na aliyetekeleza ilani hiyo ni mbunge Silvestry Koka kupitia Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan.

Wajumbe wa Mkutano Mkuu Maalum Jimbo la Kibaha Mjini uliofanyika Aprili 26,2025 na wanaoonekana mbele kutoka kulia ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Kibaha Mjini Zuhura Sekelela, Mwenyekiti wa CCM Kata ya Tangini Anthony Milao,Katibu wa CCM Kata ya Tangini Sophia Mtase,Diwani Kata ya Tangini Mfaume Kabuga na Diwani wa viti maalum Selina Wilson.

Aidha, Jumaa amesema kuwa kutokana na Maendeleo hayo ni vyema WanaCCM wakamuunga mkono Koka pamoja na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan ambaye ndiye kinara wa utoaji fedha za miradi ya maendeleo nchini.

Amesema, Koka amekuwa msaidizi mzuri wa Rais Samia kwani kila fedha inayotolewa amekuwa akiisimamia vizuri kuhakikisha inafanyakazi iliyokusudiwa na hivyo kufanya miradi ya Kibaha Mjini kukamilika kwa wakati na kuifanya Kibaha kuwa na Maendeleo makubwa.

"Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan ametekeleza ilani ya CCM nchi nzima lakini yapo maeneo yenye wabunge makini kama Kibaha Mjini mambo yamekuwa mazuri zaidi kutokana na aina ya mbunge mliyenae kwahiyo niwaombe mwaka huu tuwe kitu kimoja kumuunga mkono Rais Samia pamoja na Mbunge Koka kuhakikisha wanashinda Kwa kishindo kikubwa," amesema Jumaa



Jumaa, akizungumzia suala la ubunge amesema kuwa ubunge sio chuo cha mafunzo wala sehemu ya kujifunza kila wakati na kwamba wakifanya majaribio ni wazi kuwa watajirudisha nyuma katika suala la maendeleo na baadae wakajutia.

Amempongeza Koka kwa kazi kubwa aliyoifanya katika utekelezaji wa ilani ya CCM huku akisema Kibaha Mjini imepata  Mbunge hodari, mchapakazi na kwamba hata yeye alikaa bungeni na anamfahamu vizuri Koka na anafahamu kazi zake huku akisema ubunge sio suala la mchezo.

Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Hamoud Jumaa (MNEC)akivishwa skafu mara baada ya kuwasili katika eneo la mkutano Mkuu maalum wa Jimbo la Kibaha Mjini uliofanyika Aprili 26,2025 ikiwa ni sehemu ya uwasilishaji taarifa ya utekelezaji wa ilani ya CCM chini Mbunge wa Jimbo hilo Silvestry Koka.

Jumaa, ameongeza kuwa Koka amekuwa kiongozi mzuri ambaye amefuata nyayo za uchapakazi wa mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais Dkt .Samia Suluhu Hassan na kwamba mtu kama huyo anaweza kuwavusha vizuri katika kipindi cha 2025/2030.

Ameipongeza kamati ya siasa ya Kibaha Mjini inayoongozwa na Mwenyekiti Mwajuma Nyamka kwa kufanyakazi kubwa ya usimamizi wa utekelezaji wa ilani huku akiitaka kamati hiyo kuendelea na usimamizi huo kwa maslahi ya Wananchi wa Jimbo la Kibaha Mjini.

Jumaa, ametoa tahadhari kwa wajumbe hao kuwa makini katika kipindi hiki cha kuelekea katika uchaguzi mkuu kwani wapo wengi wanajipitisha kusaka ubunge na kutoa ahadi nyingi hivyo waangalie wasijekudanganywa.

Jumaa amewaomba wanaCCM kuunga kwa pamoja katika kipindi hiki kuchagua viongozi wazuri na wasije kuchagua viongozi kwa kufuata mitandao ambayo wakati mwingine inatumika kuchafua viongozi na ikiwezekana waache kupigana shoti.

Katibu wa Vijana wa Mkoa wa Pwani Ntoga Idd, amesema kuwa kazi aliyoifanya Koka  hakuna anayeweza kuifanya lakini yapo majimbo mengine vijana hawamjui mbunge wao lakini Kibaha Mjini Koka anajulikana kila sehemu.

Idd, amesema Koka ni mbunge sahihi kwa kuwa ni mfuatiliaji wa miradi ya maendeleo na yapo mazuri ameyafanya na yupo kwa ajili ya kuwatumikia Wananchi huku akiwataka vijana wamuunge mkono Koka kwakuwa wanataka Kibaha mpya.

Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo  la Kibaha Mjini Silvestry Koka, amesema Tanzania imepata bahati kubwa ya kumpata Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan ambaye anafanyakazi kubwa nje na ndani ya nchi.

 
Mbunge wa Jimbo la Kibaha Mjini Silvestry Koka akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa ilani ya CCM katika kipindi cha mwaka 2020/2025 kwa wajumbe wa mkutano mkuu maalum wa Jimbo la Kibaha Mjini, mkutano huo ulianza Aprili 23 na kumalizika Aprili 27,2025.

Koka, amesema mafanikio yaliyopatikana katika Jimbo lake yametokana na juhudi za Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye ndiye alikubali kutoa fedha za ujenzi wa miradi ya maendeleo Kibaha Mjini na kwamba bila yeye kusingekuwa na maendeleo.

"Mheshimiwa Rais amekuwa msikivu kwani amekuwa akishirikiana vizuri na mbunge lakini mbunge kushirikiana vizuri na Madiwani na ndio maana kazi kubwa ya ilani imeweza kufanyika ," amesema Koka

Amesema katika upande wa elimu Kibaha Mjini imepata Shule mpya za Msingi na Sekondari zaidi ya 14, vituo vya Afya, Zahanati, na miradi ya maji, umeme na huduma nyingine za kijamii zimeboreshwa.

Amesema kwasasa Kibaha Mjini imepata bahati ya kubwa ya ujenzi wa barabara za Mitaa ambazo zinakwenda kujengwa Kwa kiwango cha lami mwaka huu chini ya mradi Tactic na kwamba changamoto ya miundombinu ya barabara inakwenda kuimarika zaidi.

Koka, ameongeza kuwa mbali na barabara hizo lakini pia kwasasa upo mradi wa ujenzi wa soko kubwa la kisasa la Mnarani Loliondo na tayari fedha zimepatikana kiasi cha Sh.bilioni 18 kupitia Tactic mpango ambao unatakiwa kuanza mwaka huu.

Hatahivyo, Mwenyekiti wa CCM Kibaha Mjini Mwajuma Nyamka,Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa Jinsi ambavyo ameifanya Kibaha Mjini watembee kifua mbele kutokana na kuleta fedha nyingi za kujenga na kukamilisha miradi ya maendeleo huku akisema mbunge amekuwa mfuatiliaji mzuri.

Mwisho.


Club News Editor

Comments

Popular posts from this blog

RC PWANI AONGOZA WAKAZI PWANI KUJIANDIKISHA KWENYE DAFTARI LA WAPIGA KURA

BARAZA LA MADIWANI KIBAHA MJINI LAMPONGEZA MKURUGENZI WAKE KWA KAZI NZURI ANAYOIFANYA SAMBAMBA NA KUONGEZA MAPATO.

RAIS SAMIA ATANGAZA KIBAHA MJINI KUWA MANISAPAA,MBUNGE KOKA AFURAHIA ASEMA KIBAHA ITANG'AA