RAIS SAMIA ATOA MIKOPO ISIYO NA MASHARTI NGAZI YA KATA NCHINI

Na. Gustaphu Haule, Tanzania RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ameanzisha mpango maalum wa kutoa mikopo isiyo na masharti kwa wananchi wasiojiweza kuanzia ngazi ya Kata. Rais Samia ametoa fursa hiyo akiwalenga zaidi vijana walio na umri wa kuanzia miaka 18 hadi 45 kwa jinsia zote, wanawake na walemavu. Wanufaika wa mkopo huo watalazimika kulipa riba ndogo iliyogawanywa katika makundi matatu, ambapo kundi la vijana litalipa asilimia nne, wanawake asilimia nne na kundi la walemavu litalipa asilimia mbili. Mpango huo ni endelevu uliolenga kuwasaidia wananchi wote wenye kipato cha chini ili kujikwamua kiuchumi. Katika kuhakikisha hakuna vikwazo hatua zote za kisheria kwa wananchi kwa ajili ya kuchukua mkopo huo zimerahisishwa na hakuna kulipia gharama zozote za awali. Mkopo huu umewalenga Watanzania wa maeneo yote mijini na vijijini. Club News Editor - Charles Kusaga