MKURUGENZI KIBAHA MJINI AFUATILIA KUJIANDIKISHA VITUONI, ATEMBEA KUHAMASISHA WANANCHI


Na Gustaphu Haule,Kibaha

MKURUGENZI wa Halmashauri ya Mji Kibaha Dkt .Rogers Shemwelekwa amefanya ufuatiliaji katika vituo vya uandikishaji wa daftari la wapiga kura katika Kata mbalimbali ikiwemo  Kata ya  Kongowe, Viziwaziwa na Picha ya Ndege.

Dkt. Shemwelekwa ambaye awali aliambatana na Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakar Kunenge katika uzinduzi wa zoezi hilo Mtaa wa Mkoani" A" amelazimika kufanya ufuatiliaji huo ili kujua kama kuna changamoto katika vituo hivyo.

Akiwa katika vituo hivyo kwa wakati tofauti Dkt .Shemwelekwa alipata nafasi ya kuongea na makundi mbalimbali wakiwemo wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi ngazi ya Kata na Mitaa, Waandikishaji na Wananchi.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Kibaha Dkt.Rogers Shemwelekwa mwenye koti nyeusi akifuatilia zoezi la uandikishaji wa daftari la wapiga kura katika moja ya vituo vilivyopo katika Halmashauri yake Leo Oktoba 11.

Aidha, amewataka mawakala wa vyama vyote kuhakikisha wanafanya kazi kwa amani, utulivu na upendo vituoni mwao na kuhakikisha kila Mwananchi anapata haki ya kujiandikisha ndani ya eneo lake la makazi.

Pamoja na mambo mengine lakini mkurugenzi huyo ametumia nafasi hiyo kuwahimiza Wananchi kuendelea kujitokeza kwa ajili ya kujiandikisha ili kusudi wapate fursa ya kuchagua viongozi wao pale uchaguzi utapofika.

,"Uchaguzi wa Serikali za Mitaa unatarajiwa kufanyika Novemba 27 mwaka huu lakini kwasasa tunafanya zoezi la uandikishaji wa wapiga kura katika daftari kwahiyo niwaombe Wananchi wote ndani ya Halmashauri hii kujitokeza kujiandikisha ili wa tumie haki ya Msingi kuchagua viongozi wao wa Mitaa ,"amesema Shemwelekwa 

Mkurugenzi Halmashauri ya Mji Kibaha Dkt.Rogers Shemwelekwa (aliyesimama mwenye koti rangi nyeusi) akifuatilia hali ya uandikishaji katika moja ya  vituo vyake leo Oktoba 11 

Dkt.Shemwelekwa ameongeza kuwa ni wajibu wa kila mwananchi kupeleka ujumbe kwa mwenzake huko majumbani ili kusudi inapofika siku ya mwisho ya uandikishaji kila mwananchi hawe amefikiwa.

Hatahivyo,zoezi la uandikishaji wa daftari la Wapiga kura katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024 limeanza leo Oktoba 11, 2024 na litamalizika Oktoba 20,2024.

Baadhi ya Wananchi wakijiandikisha katika daftari  la wapiga kura katika kituo cha Mailimoja" B"kilichopo Kata ya Tangini Halmashauri ya Mji Kibaha zoezi ambalo limeanza leo Oktoba 11.


Club News Editor - Charles Kusaga

Comments

Popular posts from this blog

RC PWANI AONGOZA WAKAZI PWANI KUJIANDIKISHA KWENYE DAFTARI LA WAPIGA KURA

BARAZA LA MADIWANI KIBAHA MJINI LAMPONGEZA MKURUGENZI WAKE KWA KAZI NZURI ANAYOIFANYA SAMBAMBA NA KUONGEZA MAPATO.

RAIS SAMIA ATANGAZA KIBAHA MJINI KUWA MANISAPAA,MBUNGE KOKA AFURAHIA ASEMA KIBAHA ITANG'AA