RAIS DKT.SAMIA APAMBANIA MIUNDOMBINU YA BARABARA NCHINI, AFANIKIWA KUJENGA KILOMITA 819.22 ZA LAMI.
Na Gustaphu Haule, Tanzania
SERIKALI ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoongozwa na Rais. Dkt. Samia Suluhu Hassan, imefanikiwa kujenga barabara za lami za umbali wa Kilometa 819.22 na kuongeza za kiwango cha changarawe.
Ujenzi wa barabara hizo umeongeza mtandao wa barabara za lami kutoka kilometa 2,404.90 hadi kufikia kilometa 3,224.12.
Ujenzi wa barabara za changarawe kilometa 11,924.36 na hivyo kuongezeka kwa mtandao wa barabara za changarawe kutoka kilometa 29,183.17 hadi kilometa 41,107.52.
Mbali na ujenzi wa barabara pia Wakala wa Barabara (TARURA) wameweza kujenga madaraja makubwa sita (6) ambayo ni ya Berega (140m) (Kilosa,) Msadya (60m) (Mpimbwe DC), Mwasanga (40m) (Mbeya) ambayo tayari yameanza kutumika.
Daraja la Berega
Aidha ujenzi wa madaraja ya Kiwila (40m)-Ileje, Mkomanzi-Korogwe (60m) na Kalambo (80m)-(Kalambo), unaendelea.
TARURA imeeleza kuwa, katika kupunguza gharama, wameazimia kujenga barabara na madaraja kwa kutumia malighafi zinazopatikana maeneo ya kazi kama mawe, matofali ya kuchoma.
Kwa ujenzi wa barabara kwa kutumia mawe, mpaka sasa jumla ya kilometa 23.18 za barabara za mawe zimejengwa kwa gharama ya Shilingi Bilioni 8.1 ambapo ni sawa na Shilingi. Bilioni 12.8 kama wangetumia lami nyepesi (double surface dressing) na Shilingi. Bilioni 33.6 kama wangetumia lami ya zege (Asphat Concrete).
Ujenzi wa madaraja kwa kutumia mawe mojawapo ya kipaumbele cha TARURA ni kutumia malighafi zinazopatikana maeneo ya kazi ili kupata ufanisi wa gharama za ujenzi.
Moja ya Madaraja ya Mawe yaliyojengwa na TARURA
Hadi mwezi Februari, 2024 TARURA imejenga madaraja 226 ya mawe yenye thamani ya Shilingi Bilioni 12.52 ambapo gharama imepungua kwa zaidi ya asilimia 50.
Ujenzi wa barabara kwa kutumia tecknologia mbadala, Wakala unaendelea kufanya majaribio ya teknolojia mbalimbali ili kutumia udongo uliopo eneo la kazi badala ya kusomba kutoka maeneo mengine ya mbali.
Hadi sasa kwa kutumia Teknolojia ya ECOROADS zimejengwa Km 22 na ujenzi upo katika hatua mbalimbali za ukamilishaji.
Matengenezo ya Barabara - kilometa 21,500 zimefanyiwa matengenezo na kilometa 21,057.08 zipo katika hatua mbalimbali za ukamilishaji.
Mradi wa Agriconnect (Jumuiya ya Ulaya) - Awamu ya kwanza imekamilika ambapo km 87.6 zimejengwa kwa kiwango cha lami na katika Awamu ya Pili jumla ya km 49.12 zitajengwa.
Barabara hizo zimeongezeka kutoka kilometa 11,924.36 na kuongezeka kwa Mtandao wa barabara za changarawe toka Kilometa 29,183.17 hadi kilometa 41,107.52.
Jumla ya Shilingi Trilioni 2.53 zilitolewa na Serikali kwa ajili ya uboreshaji miundombinu ya barabara Mijini na Vijiini.
Comments
Post a Comment