WATOTO WATAJA VIBANDA UMIZA NA KAMALI VYANZO VYA UKATILI PWANI

Na. Julieth Ngarabali. Utitiri wa vibanda vya maonyesho ya video na michezo ya kamali(kubeti) maeneo mbalimbali Mkoani Pwani kumeelezwa kuwa ni baadhi ya vyanzo vinavyosababisha kuenea vitendo vya ukatili na unyanyaswaji dhidi ya watoto. Mbali na maeneo hayo pia baadhi ya waendesha bodaboda wametajwa na watoto kuwa wamekuwa wakichangia wanafunzi kukatisha masomo kwa kuwapa ujauzito . Hayo yamebainishwa baadhi ya wanafunzi kutoka shule za msingi na sekondari za Halmashauri ya mji wa Kibaha Mkoani humo kwenye mdahalo uliokuwa na lengo la kujadili masuala mbalimbali ikiwemo ya ukatili yanayowakabili watoto kuanzia umri wa miaka sefuri na kuendelea ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika Mkoani humo Katika mdahalo huo uliowashirikisha wadau mbalimbali wanaojihusisha na masuala ya watoto mada kuu tatu za ushiriki wa wadau katika kutokomeza ukatili wa jinsia ,wajibu wa wazazi na walezi katika kuwasaidia watoto kuzingatia maadil...