NITAWAPA KILA KITU ILA KADI YA CCM SITAWAPA - RIDHIWANI.



  • PIGANIENI CHAMA CHENU MSISUBIRI KUKUMBUSHWA
Na. Julieth Ngarabali. 

Naibu Waziri Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora  Ridhiwani Kikwete ambaye pia ni Mbunge wa Chalinze Pwani amewaasa vijana wa chama cha Mapinduzi kukipigania chama chao kwa wivu mkubwa ili kulinda na kutekeleza malengo ya chama katika kuwahudumia wananchi na kuleta maendeleo kwa wananchi bila ubaguzi. 


.Ridhiwani aliyabainisha hayo Mkoani Morogoro wakati akihutubia Mkutano wa Kuwaaga Wanachama wa CCM Seneti ya vyuo na tv vyuo Vikuu uliofanyika katika chuo cha Mtakatifu Jordan mkoani humo.

Amesema "hata kama ikifika siku chama hichi kinaona Ridhiwani hafai kuwa mwanachama wakaamua kunifukuza nitawapa kila kitu lakini kadi ya Chama cha Mapinduzi sitatoa kwasababu Chama cha Mapinduzi kipo moyoni mwangu na huu ndio msingi ambao mnatakiwa muwe nao , piganieni chama chenu msisubiri kukumbushwa jukumu hilo" alisisitiza Mhe. Ridhiwani




Club News Editor - Charles Kusaga

Comments

Popular posts from this blog

MWENEZI CCM PWANI AKOLEZA MOTO USIKU WA COREFA,ASIFU MAANDALIZI YAKE

WIZARA YA AFYA YASEMA:UGONJWA WA SIKOSELI SIO WA KUROGWA, YAHAMASISHA JAMII KWENDA KUPIMA VINASABA

RAS PWANI KUANZA ZIARA MANISPAA YA KIBAHA AMSIFU DKT .ROGER'S SHEMWELEKWA KWA UKUSANYAJI MAPATO