TAKUKURU PWANI YAOKOA ZAIDI YA MILIONI 314 ZILIZOKUWA ZINAPOTEA KATIKA KIZUIZI CHA MALIASILI KIBITI.
Na Gustaphu Haule ,Pwani TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Pwani imesaidia kuokoa fedha zaidi ya Sh.milioni 314 zilizokuwa zinapotea kwa mwaka katika Kizuizi cha Maliasili kilichopo Wilayani Kibiti. Awali kabla Takukuru hawajafanya ufuatiliaji katika Kizuizi hicho makusanyo ya mapato kwa wiki kwa kutumia mashine ya POS yalikuwa kiasi cha Sh.milioni 4.6 ambapo kwa mwaka ukusanya kiasi cha Sh.milioni 166.7. Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Pwani Alli Sadiki, amewaambia Waandishi wa habari Januari 31, 2025 katika mkutano uliofanyika ofisini kwake Mjini Kibaha kuwa walifanya ufuatiliaji katika kituo hicho na kubaini fedha nyingi kupotea katika Kizuizi hicho. Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Pwani Alli Sadiki, akizungumza na Waandishi wa habari Januari 31,2025 katika ofisi zake zilizopo Mjini Kibaha kuhusu utekelezaji wa shughuli za taasisi zilizofanyika katika kipindi cha Oktoba hadi Desemba 2024. Sadiki, amesema kuwa katika kipindi cha Oktoba na Desemba 2024 Takukuru ...