COREFA YAUNDA KAMATI ,YATEUA WALEZI KUENDELEZA SOKA ,YAJINASIBU "PWANI LAZIMA MPIRA UCHEZWE"


Na Gustaphu Haule,Pwani

CHAMA cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Pwani (COREFA) kimeunda kamati  mbalimbali sambamba na kuteua walezi mahususi kwa ajili ya kusimamia na kuendeleza michezo katika maeneo yote ndani ya  Mkoa.

Kamati hizo zimeundwa Januari 25 kufuatia kikao cha Kamati ya utendaji kilichoketi katika ukumbi wa Seven Seven uliopo The Art Hotel Kibaha MiembeSaba.

Mwenyekiti wa Chama Cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Pwani (COREFA) Robert Munisi, ametangaza kamati hizo mbele ya viongozi wa FA kutoka Wilaya  zote  katika mkutano maalum na kwanza wa COREFA ulioitishwa kwa ajili ya kupeana miongozo ya  namna ya kuendeleza Soka la Pwani.

Mwenyekiti wa Chama Cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Pwani (COREFA) Robert Munisi akizungumza na viongozi wa FA katika mkutano maalum uliofanyika The Art Hotel (Seven Seven) Januari 25 mwaka huu.

Katika mkutano huo Munisi, amesema COREFA tayari mpaka sasa imeunda kamati Sita ikiwemo kamati ya fedha na mipango iliyo chini ya mwenyekiti wake Mohamed Lacha,Kamati ya Vijana, Wanawake na Soka la Ufukweni(Beach Soccer) iliyochini ya mwenyekiti wake Asha Mbatta.

Munisi, ametaja kamati nyingine kuwa ni kamati ya Miundombinu chini ya mwenyekiti wake Rugemalira Rutatina,Kamati ya mashindano chini ya Nassoro Mbilinyi,kamati ya tuzo na zawadi chini ya mwenyekiti Elnuru Mmary pamoja na kamati ya uendeshaji ligi iliyochini ya Abdallah Simba.

Katika hatua nyingine COREFA imefanya uteuzi wa walezi mbalimbali kwa ajili ya kusimamia FA za Wilaya zilizopo ndani ya Mkoa ambapo miongoni mwa walezi hao ni Elnuru Mmary aliyepewa Wilaya ya Bagamoyo.

Mkutano wa Chama Cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Pwani(COREFA) uliofanyika Januari 25 ,2025 katika ukumbi wa Seven Seven uliopo The Art Hotel Kibaha MiembeSaba ukiwa na lengo la kupeana miongozo ya uendeshaji wa Soka la Pwani.

Munisi , amesema walezi wengine ni Nassoro Mbilinyi aliyepewa FA ya Wilaya ya Mkuranga, Mohamed Lacha (Mafia), Rugemalira Rutatina (Kisarawe), Asha Mbatta(Kibaha), Abdallah Simba (Kibiti) na Mohamed Masenga akipewa ulezi wa FA ya Wilaya ya Rufiji.

Aidha, Munisi amesema kuwa lengo la kuunda kamati na kuteua walezi hao ni kutaka kuhakikisha wanasimamia kikamilifu kauli Mbiu ya COREFA inayosema "Pwani lazima Mpira Uchezwe" ambapo kupitia kamati na walezi hao kila FA itakuwa inawajibika na kuwasiliana na walezi hao katika kutatua changamoto zote za michezo katika maeneo yao.

Hatahivyo, Munisi amewataka viongozi wa FA kushirikiana vyema na walezi hao na ikiwezekana kila mmoja awajibike katika nafasi yake ili kusudi Mpira wa Pwani ufike mbali ikiwa pamoja na kuibua vipaji vya michezo kwa vijana.

Mwisho 
Club News Editor

Comments

Popular posts from this blog

RC PWANI AONGOZA WAKAZI PWANI KUJIANDIKISHA KWENYE DAFTARI LA WAPIGA KURA

BARAZA LA MADIWANI KIBAHA MJINI LAMPONGEZA MKURUGENZI WAKE KWA KAZI NZURI ANAYOIFANYA SAMBAMBA NA KUONGEZA MAPATO.

RAIS SAMIA ATANGAZA KIBAHA MJINI KUWA MANISAPAA,MBUNGE KOKA AFURAHIA ASEMA KIBAHA ITANG'AA