SERIKALI YA RAIS SAMIA YAONDOA MALALAMIKO YA WAGONJWA ULANGA.
Na Gustaphu Haule, Tanzania #KAZIINAONGEA HATUA ya Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan ya kukamilisha ujenzi wa kituo cha kupoza umeme cha Ifakara imesaidia kwa kiasi kikubwa kuondoa malalamiko ya wananchi ya kuchelewa kupata huduma za afya kwenye hospitali ya Wilaya ya Mahenge. Kituo cha kupoza umeme cha Ifakara Hayo yamethibitishwa na Katibu wa afya Hospitali ya Wilaya ya Ulanga, Goodluck Malya ambae amesema kabla ya kuwepo kwa huduma ya nishati kutoka kwenye kituo hicho hali ilikuwa ni mbaya kwani kuna huduma zilikuwa hazipatikaniki lakini pia gharama za nishati zilikuwa za juu kutokana na kutumia genereta. "Toka kuwashwa kwa kituo cha kupoza umeme Ifakara hospitali ya wilaya ya Ulanga imeona mabadiliko makubwa kwa huduma mbalimbali zinazotegemea nishati ya umeme zimekuwa na mafanikio makubwa,"amesema Malya "Awali kuna mambo yalikuwa hayawezi kufanyika na hospitali ilikuwa ikiingia gharama kubwa katika shughuli za uendeshaji hasahasa katika nishati ya umeme lakini b...