MAFANIKIO YA RAIS DKT.SAMIA KATIKA USAFIRI WA TRENI YA SGR YAONEKANA.



Na Gustaphu Haule, Tanzania 

*● Imesafirisha abiria zaidi ya 1,000,000 katika kipindi cha miezi minne*

# KAZIINAONGEA

MAFANIKIO makubwa yaliyotokana na jitihada za Rais wa awamu ya tatu Dkt.Samia Suluhu Hassan tangu alipoingia madarakani yameonekana hasa katika kuleta unafuu mkubwa kwa Watanzania kwenye suala zima la usafiri wa Treni ya umeme (SGR) kutoka Dar es Salaam kwenda Morogoro na Dodoma.


Kuanzishwa kwa usafiri huo kumesaidia kutoa unafuu katika Sekta ya usafiri ambapo pia Shirika la Reli Tanzania (TRC) limefanikiwa kusafirisha abiria zaidi ya 1,000,000 katika kipindi cha miezi minne tangu uzinduzi wa njia ya Treni za umeme kati ya Dar es Salaam na Dodoma, mnamo Juni 2024.

Idadi hiyo ni mara mbili ya abiria waliosafirishwa na Treni ya zamani (MGR) ambayo ilisafirisha jumla ya abiria 400,000 katika kipindi cha mwaka mmoja ambapo kuanzishwa kwa treni ya SGR kumefanya idadi ya abiria wa Treni hiyo kuongezeka siku hadi siku.


  



Shirika hilo la Reli (TRC) inatambua umuhimu wa huduma  hii ya kisasa katika kuboresha usafiri ambao unatumia muda mfupi hivyo kuharakisha huduma za kijamii na kiuchumi.

TRC pia inatambua umuhimu wa huduma hii katika kuongeza ufanisi wa biashara na kutoa chaguo la haraka na la salama kwa abiria katika usafiri huo wa Treni za Mwendokasi zinazotumia umeme.

Katika kuboresha huduma hiyo ya kisasa, TRC imepanga kuongeza huduma na kuboresha miundombinu ya SGR ili iweze kuendelea kutoa huduma yenye tija zaidi.



Uwekezaji katika Reli ya Standard Gauge (SGR) imefanikiwa kuingiza mapato Taifa ya takriban Shilingi Bilioni 16 zilizozalishwa katika kipindi cha miezi minne tangu kuanzishwa kwa reli hiyo ya huduma za treni za umeme.
kupitia sekta ya Uchukuzi .

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alipoingia madarakani ujenzi wa SGR ulikuwa ni kipande cha kwanza na kipande cha pili ambapo hadi sasa tayari ujenzi wa reli hiyo umekamilika na safari inaanza kutoka Dar es Salaam - Morogoro hadi Dodoma.



Kutokana na jitihada hizo Watanzania wanatakiwa kujivunia na kuanza kuona fursa za kiuchumi zilizoko kupitia reli ya SGR na kubuni mbinu za kibiashara kati ya Tanzania na nchi tunazopakana nazo Kama Demokrasia ya Kongo, Rwanda, Burundi, Uganda, Malawi na Zambia.

Kwa Bara la Afrika reli ya SGR ndio reli ndefu kuliko zote na reli hii ya hapa nchini ndo reli ndefu ya takribani kilomita za ujenzi 2102, katika Afrika ndio nchi pekee inajenga reli ndefu na ya bei nafuu na ya kisasa na imeweza kuongeza ufanisi katika uzalishaji haswa katika sekta ya Biashara.

#KAZIINAONGEA

Club News Editor

Comments

Popular posts from this blog

RC PWANI AONGOZA WAKAZI PWANI KUJIANDIKISHA KWENYE DAFTARI LA WAPIGA KURA

BARAZA LA MADIWANI KIBAHA MJINI LAMPONGEZA MKURUGENZI WAKE KWA KAZI NZURI ANAYOIFANYA SAMBAMBA NA KUONGEZA MAPATO.

RAIS SAMIA ATANGAZA KIBAHA MJINI KUWA MANISAPAA,MBUNGE KOKA AFURAHIA ASEMA KIBAHA ITANG'AA