TAKUKURU YATOA ONYO KWA WAPIGA KURA NA WAGOMBEA UCHAGUZI SERIKALI YA MTAA





Na Gustaphu Haule, Tanzania 

#KAZIINAONGEA

SERIKALI ya awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan imewaonya wapiga kura na wagombea kuacha kujihusisha na vitendo vya rushwa  kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Vijiji na Vitongoji unaotarajiwa kufanyika Novemba 27,2024.

Hitaji la Rais Samia ni kuona kunakuwa na uchaguzi wa huru na haki bila kujali ni mgombea wa chama gani atashinda.

Kwa kulifanikisha hilo Novemba 26,2024, Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Ilala imesema itachuka hatua kwa yeyote atayepokea ,kutoa au kujihusisha na rushwa.

Hayo ameyasema Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Ilala Sosthness Kibwengo wakati akizungumza na waandishi wa habari Dar es salaam.

"Uchaguzi ni maisha uchaguzi ni maendeleo tunaelekea katika uchaguzi wa serikali za mitaa tufahamu kwamba rushwa ni kikwazo katika maendeleo, rushwa ni kikwazo kufanya uchaguzi ambao upo sahihi, rushwa ni kikwazo katika kukuwezesha wewe katika kuchagua kiongozi ambaye ni bora,"amesema Kibwengo

"Katika kuwakumbusha wananchi tumefanya vipindi 41 vya redio, tumefanya zaidi ya mikutano 69 ya hadhara, tumefanya semina 33 kwa makundi mbalimbali ikiwamo semina ya viongozi wetu wa dini ambao tuliwaomba walisemee jambo hilo kwenye nyumba za dini na kuwataka watu wajue umuhimu wa kuzingatia maadili katika suala la uchaguzi," amesema Kibwengo

Aidha Kibwengo amesema uchaguzi huu ni muhimu hivyo wananchi wajitokeze na wachague viongozi sahihi kwa maendeleo ya nchi.

#KAZIINAONGEA

Club News Editor

Comments

Popular posts from this blog

RC PWANI AONGOZA WAKAZI PWANI KUJIANDIKISHA KWENYE DAFTARI LA WAPIGA KURA

BARAZA LA MADIWANI KIBAHA MJINI LAMPONGEZA MKURUGENZI WAKE KWA KAZI NZURI ANAYOIFANYA SAMBAMBA NA KUONGEZA MAPATO.

RAIS SAMIA ATANGAZA KIBAHA MJINI KUWA MANISAPAA,MBUNGE KOKA AFURAHIA ASEMA KIBAHA ITANG'AA