MBONI MKOMWA: NITAJENGA SHULE YA MSINGI NA ZAHANATI MTAA WA BAMBA,WANANCHI NICHAGUENI





Na Gustaphu Haule,Pwani 

MBONI Mkomwa ni mgombea wa nafasi ya mwenyekiti katika Serikali ya Mtaa wa Bamba Kata ya Kongowe katika Halmashauri ya Mji Kibaha Mkoa wa Pwani.

Mboni, anaingia katika kinyang'anyiro cha nafasi hiyo kwa mara ya kwanza licha ya kuwa awali alikuwa mjumbe wa Serikali ya Mtaa huo kwa muda wa miaka mitano iliyopita.

Uzoefu wa Mboni katika kutumikia nafasi hiyo kumempa uzoefu mkubwa katika uongozi na hivyo kuona anaweza kuongoza Mtaa huo kwa nafasi ya mwenyekiti.

Kwasasa Mboni (39) ni Mjane na mama wa watoto watatu anayejishughulisha na biashara ndogondogo ambayo kwa kiasi kikubwa ndio inayompa kipato cha kuendesha maisha.

Katika mahojiano yake na mwandishi wa makala haya katika moja ya mikutano yake ya kampeni Mboni anaanza kwa kukishukuru Chama Cha Mapinduzi (CCM)kwa kumuamini na kumpa nafasi ya kupeperusha bendera ya Chama hicho.


Amesema, mbali na chama hicho lakini pia anawashukuru wanachama wa CCM pamoja na wananchi mbalimbali wa Mtaa wa Bamba kwa kumpa moyo na kuridhia aingie kugombea katika nafasi hiyo .

Amesema kwasasa ameingia kugombea nafasi hiyo ili kuhakikisha anapambana na changamoto zilizopo katika Mtaa wake ili kusudi Wananchi wake waweze kupata huduma za kijamii kwa urahisi.

Mboni, amesema kuwa akishinda katika nafasi hiyo atahakikisha Mtaa wake unapata Shule mpya ya Msingi ili kuwapa nafasi watoto kusoma katika mazingira mazuri zaidi.


Mboni, amesema kwasasa Mtaa huo hauna Shule ya Msingi jambo ambalo linasababisha wanafunzi waliopo katika Mtaa huo kulazimika kuvuka barabara ya Morogoro kwa ajili ya kufuata Shule katika Mtaa mwingine wa jirani.

Amesema kitendo cha kukosa Shule hiyo ni wazi kuwa inaleta kero kwa wanafunzi hao kusoma katika mazingira magumu jambo ambalo wakati mwingine linakatisha tamaa ya kusoma.


Amesema kuwa, mbali na ukosefu wa Shule lakini anatambua kuwa zipo changamoto nyingine ndani ya Mtaa wake zinazohitaji kupata ufumbuzi wa haraka.

"Natambua changamoto zilizopo katika Mtaa wangu ndio maana nikajitokeza kugombea ili niweze kuzitafutia ufumbuzi wa kina na hivyo kupunguza adha wanayoipata Wananchi wangu," amesema Mboni.

Mboni amesema moja ya changamoto hizo ni ukosefu wa Zahanati,ubovu wa miundombinu ya barabara pamoja na kuwepo kwa mikopo kausha damu inayowasumbua Wanawake.

Amesema, akiwa mwenyekiti atashirikiana na viongozi wenzake pamoja na wananchi wa Mtaa ili kuhakikisha wanaweka mipango ya pamoja kwa ajili kutatua changamoto zilizopo katika Mtaa wao.

Kuhusu ujenzi wa Zahanati hiyo Mboni amesema kuwa kwasasa Wananchi wake wanatumia kituo cha afya Kongowe kilichopo mbali na maeneo yao jambo ambalo ni kero kwa Wananchi.

Amesema, akishaingia madarakani pamoja na mambo mengine atahakikisha pia ndani ya uongozi wake Zahanati inapatikana ili kuleta urahisi wa Wananchi kupata huduma ya matibabu ya afya.

Kwa upande wa changamoto ya barabara atashirikisha viongozi na wananchi kwa kuunda kamati maalum ambayo itakuwa inafanyakazi kwa karibu na Wakala wa Barabara Mijini na Vijijini (TARURA).

Mboni, amesema barabara zote zenye vigezo vya kuingia katika mpango wa TARURA lazima atasimamia kwa karibu ili zipate nafasi ya kuhudumiwa mara kwa mara lakini zile ambazo zitakuwa ndani ya Wananchi wenyewe nazo zitatengenezewa mpango maalum .

"Wananchi wenzangu wa Mtaa wa Bamba naomba kura zenu, mnichague mimi kuwa mwenyekiti wenu nami nitawalipa mafanikio na matokeo mazuri kwani nipo tayari kufanyakazi usiku na mchana kwa ajili ya kupigania maendeleo ya Mtaa wetu ,"amesema Mboni.

Aidha ,Kuhusu Wanawake wenzake Mboni amesema kuwa wakimchagua watakuwa wamepata mwakilishi mzuri atakayekwenda kuwasimamia katika  masuala yao ya kiuchumi hususani suala la mikopo .

Amesema moja ya jukumu atakalofanya ni kuhakikisha anawasaidia  Wanawake kuondokana na mikopo kausha damu ambayo inawafanya wakose usingizi.

"Natambua sisi Wanawake tunaumizwa sana na mikopo kausha damu kwahiyo mimi Mboni mkinichagua kazi yangu ni kuhakikisha nakwenda kuwatengenezea mazingira mazuri ili mkanuifaike na mikopo inayotolewa na Halmashauri", amesema Mboni

Ameongeza kuwa Halmashauri ya Mji Kibaha inatoa mikopo ya asilimia 10 kwa Wanawake,Vijana na Watu wenye ulemavu lakini wengi bado hawana uelewa wa namna ya kuomba mikopo hiyo lakini kazi hiyo kwasasa ataifanya pale atakapochaguliwa.

Mboni amewaomba wakazi wote wa Mtaa huo ifikapo Novemba 27 kwenda katika vituo vya kupigia kura na bila makosa wamchague ili aweze kushinda kwa kishindo na hivyo kuleta maendeleo.

Kata ya Kongowe inajumla ya Mitaa Sita ambapo kati ya Mitaa hiyo Wanawake wanaogombea nafasi ya mwenyekiti ni wawili akiwemo Mboni Mkomwa kutoka Mtaa wa Mbamba na Nuru Awadhi kutoka Mtaa wa MiembeSaba" B "
 



Club News Editor

Comments

Popular posts from this blog

RC PWANI AONGOZA WAKAZI PWANI KUJIANDIKISHA KWENYE DAFTARI LA WAPIGA KURA

BARAZA LA MADIWANI KIBAHA MJINI LAMPONGEZA MKURUGENZI WAKE KWA KAZI NZURI ANAYOIFANYA SAMBAMBA NA KUONGEZA MAPATO.

RAIS SAMIA ATANGAZA KIBAHA MJINI KUWA MANISAPAA,MBUNGE KOKA AFURAHIA ASEMA KIBAHA ITANG'AA