Posts

Showing posts from November, 2023

HOSPITALI YA RUFAA TUMBI YATOA HUDUMA YA MACHO BURE

Image
  Na Gustafu Haule, Pwani   Hospitali ya Rufa ya Mkoa wa Pwani Tumbi iliyopo Kibaha Mkoani Pwani kwa kushirikiana na taasisi ya Qatar Charity imetoa huduma ya upimaji na upasuaji wa macho bure Kwa wananchi zaidi ya 1000 waishio katika maeneo mbalimbali ya mkoa huo.   Huduma hiyo ilianza kutolewa Novemba 15 mwaka huu na kumalizika Novemba 18 ambapo katika huduma hiyo wananchi walipimwa macho na yeyote aliyebainika kuwa na tatizo alipata dawa na wengine kufanyiwa upasuaji bure .   Pichani watoa huduma katika Hospitali ya Rufaa Tumbi wakiwa wamejipanga kwa ajili ya kutoa huduma kwa Wananchi Daktari Bingwa wa Macho   katika hospitali hiyo Dr.Mathew Yinza, amesema kuwa toka wameanza kutoa huduma hiyo Novemba 15 imekuwa na mwitikio mkubwa wa wananchi kwani mpaka Sasa zaidi ya wananchi 1000 wamejitokeza na kupata huduma.   Dr. Nyinza, amesema kuwa mwananchi anayepimwa na kugundulika na ugonjwa wa macho anapata huduma kulingana na hali yake jinsi il...

KAMATI YA BUNGE UWEKEZAJI NA MITAJI YA UMMA YASHIRIKIANA NA RC KUNENGE KUKAGUA MITAMBO YA MAJI YA DAWASA WAMI .

Image
  Na Gustafu Haule,Pwani   Kamati   ya Bunge ya Uwekezaji na   Mitaji ya Umma pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mh. Abubakar Kunenge wamefanya ziara ya kutembelea na kukagua mitambo ya uzalishaji maji ya Dawasa iliyopo Wami   Chalinze Mkoani Pwani.   Katika ziara hiyo iliyofanyika Novemba 12 mwaka huu kamati hiyo iliambatana na viongozi wengine akiwemo Naibu Waziri Ofisi ya Rais,Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Ridhiwani Kikwete,Katibu Mkuu Wizara ya Maji Jamal Katundu ,Mkurugenzi Mkuu wa Dawasa Kiula Kingu,pamoja na baadhi ya watumishi wa Dawasa.   Wakiwa katika mitambo hiyo wajumbe wa kamati hiyo wakiongozwa na mwenyekiti wao Deus Sangu ,walipokea taarifa ya utekelezaji wa mradi huo kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Dawasa Kiula Kingu na baadae kutembelea sehemu mbalimbali za uchakataji wa maji hayo.   Kingu,amesema kuwa mradi wa maji Wami umetekelezwa kwa awamu tatu ambapo mpaka sasa umetumia zaidi ya bilioni 160 na kwa...

VIFO VITOKANAVYO NA MATATIZO YA UZAZI VIMEPUNGUA KATIKA HOSPITALI YA RUFAA MKOA WA PWANI

Image
  Na. Julieth Ngarabali,   Pwani.   Vifo vya wajawazito   vitokanavyo   na matatizo   ya uzazi   vimepungua kutoka   vitano kwa mwaka 2021 hadi vitatu kwa mwaka huu 2023 katika hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Pwani ya Tumbi na kwamba lengo ni kutokuwa na kifo kwa kipindi kijacho.   Takwimu hizo ni za hospitalini   humo   ambapo   imeelezwa ni sehemu ya mafanikio ya jitihada mbalimbali zinazofanywa na Serikali pamoja na wadau ya kupunguza kabisa ama kufuta vifo vya wazazi vitokanavyo na matatizo ya uzazi.   Akizungumza kwenye ufunguzi wa mbio za Coast City Marathon zilizofanyika Kibaha Mkoa wa Pwani kwa niaba ya Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu, Mkuu wa mkoa wa Pwani, Mh. Abubakari Kunenge amesema Serikali imekuwa ikipambana na vifo vya mama na mtoto na changamoto zilizopo ambapo Wizara ya afya imeendelea kupambana nazo kuhakikisha zinaisha na huduma zinaboreshwa .               ...

RC KUNENGE AWAPA MAAGIZO MAZITO KWA WAKURUGENZI ,WAKUU WA WILAYA ,AWATAKA KUYATAMBUA MASHAMBA PORI.

Image
  Na Gustafu Haule,Pwani   MKUU wa Mkoa wa Pwani Mh. Abubakar Kunenge, ametoa maagizo kwa Wakuu wa Wilaya pamoja na Wakurugenzi wa Halmashauri kuhakikisha wanafanya utambuzi wa mashamba pori yasiyoendelezwa ili wahusika wachukuliwe hatua za kisheria.   Kunenge,ametoa maagizo hayo katika mkutano wake na waandishi wa habari uliowajumuisha   Wakurugenzi na Wakuu wa Wilaya uliofanyika Mjini Kibaha kuhusu namna Serikali ilivyojipanga kukabiliana na migogoro ya ardhi.   Kunenge,amesema kuwa Mkoa wa Pwani bado kuna mashamba pori mengi na makubwa ambayo yametelekezwa na watu bila kuyafanyiakazi na hivyo kuathiri uzalishaji kwa watu wa Mkoa wa Pwani.   Amesema,mbali na hilo lakini wakati mwingine mashamba hayo yanatumika kama vichaka vya kufanyia matendo ya uhalifu jambo ambalo Serikali haiwezi kukubali hali hiyo iendelee.   Kunenge, ameongeza kuwa baada ya kufanya utambuzi huo hatua itakayofuata ni kuwaandikia barua wahusika wa mashamba hay...

MAAFISA UTPC WAFANYA ZIARA MKOA WA PWANI

Image
Maafisa Program wa Umoja wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC) wamefanya ziara Mkoa wa Pwani katika Ofisi za Klabu ya Waandishi wa habari mkoa wa Pwani (CRPC) zilizopo Mailimoja Kibaha. Ziara hiyo ni moja kati ya malengo ya kuimarisha utendaji kazi wa Klabu za Waandishi wa habari nchini katika dhana ya kutoka hatua bora kwenda hatua bora zaidi ya kulinda na kuendeleza tasnia ya habari nchini.   Pichani sehemu ya Uongozi wa Klabu CRPC pamoja na Maafisa toka UTPC katika kikao kazi kujadili utendaji kazi wa Klabu. Mambo muhimu yaliyozingatiwa katika ziara hii kuangalia namna Klabu inavyopaswa kujipambanua na kuweza kuonyesha umuhimu wake ili iwe na tija katika tasnia ya habari katika kila mkoa. Pia ziara hiyo iliangalia mifumo ya Utawala na Fedha ili kuleta uwajibikaji mzuri katika rasilimali za Klabu.   Afisa Program Ndugu Victor Maleko akifafanua jambo katika kikao kazi kati ya Uongozi wa  Klabu CRPC na UTPC Umoja wa Klabu za Waandishi wa habari Tanzania ...

MSEMAJI MKUU WA SERIKALI ANENA MAZITO, ATAKA WAKURUGENZI WAELEZE MAFANIKIO YA UTEKELEZAJI WA MIRADI

Image
    Na Gustafu Haule, Pwani.   MKURUGENZI wa Idara ya Habari Maelezo na Msemaji Mkuu wa Serikali Mobhare Matinyi amewashauri viongozi wa Serikali kuhakikisha wanawaelezea wananchi miradi iliyotekelezwa katika maeneo yao ili kuondoa sintofahamu baina ya wananchi na Serikali yao. Matinyi amebainisha   hayo jana katika mkutano wake uliofanyika Mjini Kibaha na kuhusisha viongozi mbalimbali akiwemo Mkuu wa Mkoa huo Abubakar Kunenge, Wakuu wa Wilaya, viongozi wa mkoa huo pamoja na Wakurugenzi wa Halmashauri.   Amesema, Serikali imekuwa ikipeleka fedha nyingi za miradi ya Maendeleo kwa ajili ya maslahi ya wananchi   lakini wananchi hawaelezwi michanganuo na mengine ambayo yamefanywa na serikali.   Aidha, amesema viongozi wa mikoa wanatakiwa kusimamia fedha za utekelezaji wa miradi hiyo ili iweze kuleta matokeo chanya kwa wananchi sambamba na kuwashirikisha kwa kila hatua kwenye maeneo husika.   Akielezea kuhusu mkutano huo amesema ni ...

MAONYO JUU YA KUKITHIRI KWA VITENDO VYA UKATILI NA UKANDAMIZAJI DHIDI YA WAANDISHI WA HABARI

Image
 Na. Mwandishi Wetu. Raisi wa Muungano wa Klabu za Waandishi wa habari Tanzania Bw. Deogratius Nsokolo ametoa wito kwa umma kuelimishwa juu ya umuhimu wa uhuru wa vyombo vya habari na nafasi ya Waandishi wa habari katika jamii.   Ameyazungumza hayo wakati akifungua Mkutano wa Maadhimisho ya siku ya Kimataifa ya kukomesha uhalifu dhidi ya Waandishi wa habari ulioendeshwa kwa njia ya mtandao (Zoom Meeting).   Maadhimisho hayo kwa Mwaka 2023 yamelenga kuongeza uelewa kuhusu changamoto wanazokabiliana nazo Waandishi wa habari katika kutekeleza majukumu yao, na pia kuonya juu ya kukithiri kwa vitendo vya ukatili na ukandamizi dhidi ya Waandishi wa habari.   Katika hotuba yake ameelezea mambo muhimu katika jamii kama   Kuimarisha Demokrasia, kulinda haki za Binadamu na   kujenga Mazingira salama kwa Waandishi wa habari.

WATU WATANO WAFA MAJI AJALINI MAFIA MKOA WA PWANI

Image
  Na. Julieth Ngarabali. Pwani.     Watu watano wamefariki Dunia kwa kuzama majini na wengine wawili hawajulikani walipo baada ya boti waliokua wanasafiria kwa shughuli za uvuvi Wilayani Mafia Mkoani Pwani kugonga kingo za mto Rufiji na kupinduka baharini Wilayani humo.   Boti hiyo ilikua imebeba watu 15 wanaojishughulisha na shughuli za uvuvi kutoka Mafia kwenda Kibiti ambapo kati yao nane   tayari wameokolewa wazima.   Mkuu wa Wilaya ya Mafia Mh. Zephania Sumaye akizungumza kwa njia ya simu Leo Jumatano Novemba mosi amesema boti hiyo ya uvuvi ilianza safari juzi mchana ikitoka eneo la Kimbugi   Mafia kuelekea eneo la Bwera Kibiti ikiwa na watu 15   ambao wanaume ni 12 na wanawake watatu wote wanajishughulisha na shughuli za uvuvi.   "Ilipata ajali katika kingo za mto Rufiji baada ya boti hiyo kujigonga katika kuta za mto Rufiji Jana mchana, kwa hiyo sisi saa nane mchana tulipata taarifa hizi na kwa sababu tulikua tumeshajian...