MAAFISA UTPC WAFANYA ZIARA MKOA WA PWANI
Maafisa Program wa Umoja wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC) wamefanya ziara Mkoa wa Pwani katika Ofisi za Klabu ya Waandishi wa habari mkoa wa Pwani (CRPC) zilizopo Mailimoja Kibaha. Ziara hiyo ni moja kati ya malengo ya kuimarisha utendaji kazi wa Klabu za Waandishi wa habari nchini katika dhana ya kutoka hatua bora kwenda hatua bora zaidi ya kulinda na kuendeleza tasnia ya habari nchini.



Pichani
sehemu ya Uongozi wa Klabu CRPC pamoja na Maafisa toka UTPC katika kikao kazi
kujadili utendaji kazi wa Klabu.
Mambo muhimu yaliyozingatiwa katika ziara hii kuangalia namna Klabu inavyopaswa kujipambanua na kuweza kuonyesha umuhimu wake ili iwe na tija katika tasnia ya habari katika kila mkoa. Pia ziara hiyo iliangalia mifumo ya Utawala na Fedha ili kuleta uwajibikaji mzuri katika rasilimali za Klabu.
Klabu CRPC na UTPC
Umoja wa Klabu za Waandishi wa habari Tanzania kupitia Klabu za mikoa upo katika mabadiliko ya kupiga hatua bora zaidi kiutendaji katika kauli mbiu "Moving from Good to Great " ili kuweka mazingira mazuri kiutendaji kuleta tija zaidi katika tasnia ya habari kwa Umma na jamii.
Comments
Post a Comment