MAONYO JUU YA KUKITHIRI KWA VITENDO VYA UKATILI NA UKANDAMIZAJI DHIDI YA WAANDISHI WA HABARI
Na. Mwandishi Wetu.
Raisi wa Muungano wa Klabu za Waandishi wa habari Tanzania Bw. Deogratius Nsokolo ametoa wito kwa umma kuelimishwa juu ya umuhimu wa uhuru wa vyombo vya habari na nafasi ya Waandishi wa habari katika jamii.
Ameyazungumza hayo wakati akifungua Mkutano wa Maadhimisho ya siku ya Kimataifa ya kukomesha uhalifu dhidi ya Waandishi wa habari ulioendeshwa kwa njia ya mtandao (Zoom Meeting).
Maadhimisho hayo kwa Mwaka 2023 yamelenga kuongeza uelewa kuhusu changamoto wanazokabiliana nazo Waandishi wa habari katika kutekeleza majukumu yao, na pia kuonya juu ya kukithiri kwa vitendo vya ukatili na ukandamizi dhidi ya Waandishi wa habari.
Katika hotuba yake ameelezea mambo muhimu katika jamii kama Kuimarisha Demokrasia, kulinda haki za Binadamu na kujenga Mazingira salama kwa Waandishi wa habari.
Comments
Post a Comment