KOKA ASHINDA UCHAGUZI KURA ZA MAONI CCM KIBAHA ANYAKUA KURA 2,824
Na Gustaphu Haule, Pwani
Mbunge mstaafu wa Jimbo la Kibaha Mjini Silvestry Koka akipiga kura Katika uchaguzi wa kura za maoni za Chama Cha Mapinduzi (CCM) uliofanyika Agosti 4 Kata ya Tumbi.
Club News Editor
Mbunge mstaafu wa Jimbo la Kibaha Mjini Silvestry Koka amefanikiwa kushinda katika uchaguzi wa kura za maoni kwa kupata kura 2,824 na kuwaacha mbali wengine watano waliokuwa wakipambania nafasi hiyo.
Akitangaza matokeo hayo mara baada ya uchaguzi wa kura za maoni uliofanyika Agosti 4, 2025 Katibu wa CCM Kibaha Mjini Isaack Kalleiya amemtangaza Koka kuwa ni mshindi aliyeongoza kwa kupata kura nyingi zaidi.
.
Kalleiya,amesema Kibaha Mjini inakata 14 na jumla ya wajumbe 6300 walipaswa kupiga kura katika uchaguzi huo lakini kura zilizopigwa ni 5,743, zilizoharibika 53 na kura halali 5,682.
Amesema katika matokeo hayo Koka ameongoza kwa kupata kura 2,824,akifuatia na Musa Mansour aliyepata kura (1,775), Abubakar Allawi aliyepata kura (727),Dkt.Charles Mwamwaja( 282), Magreth Mwihava (39) na Ibrahim Mkwilu (35).
Kalleiya amesema kuwa chama kinautaratibu wake na mara baada ya taratibu hizo kukamilika miongozo mingine itafuata.
Kwa upande wake Koka amewashukuru wajumbe kwa kumchagua na kumpa heshima kubwa ya kuwa mshindi katika uchaguzi huo na kwamba kilichobaki ni taratibu zingine za chama .
Hatahivyo, uchaguzi wa kura za maoni katika Jimbo la Kibaha Mjini kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) uliofanyika katika Kata 14 .
MWISHO.
Comments
Post a Comment