HAMOUD JUMAA AJIZOLEA KURA 3,247 AONGOZA UCHAGUZI KURA ZA MAONI
Na Gustaphu Haule,Pwani
MJUMBE wa Halmashauri Kuu ya Taifa kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Hamoud Jumaa (MNEC) amefanikiwa kumbwaga aliyekuwa mbunge wa Jimbo la Kibaha Vijijini Michael Mwakamo kwa kupata kura 3,247.
Hamoud ameshinda katika uchaguzi wa kura za maoni wa ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) uliofanyika Agosti 4, 2025 katika Jimbo la Kibaha Vijijini lililopo Mkoani Pwani.
Mgombea aliyeshinda katika uchaguzi wa kura za maoni za Chama Cha Mapinduzi (CCM)katika Jimbo la Kibaha Vijijini Hamoud Jumaa.
Uchaguzi wa kura za maoni umefanyika kwa ajili ya kutoa nafasi kwa wajumbe wa mkutano mkuu wa Jimbo la Kibaha Vijijini kwa ajili ya kumpata mwakilishi wa kugombea ubunge katika uchaguzi mkuu unaotarajia kufanyika Oktoba 29 mwaka huu.
Katibu wa Siasa, Uenezi na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi ( CCM) Mkoa wa Pwani David Mramba ametoa taarifa hizo katika mkutano na Waandishi wa habari uliofanyika leo Agosti 5,2025 katika Ofisi za CCM Mkoa wa Pwani.
Mramba ,amesema kuwa katika Jimbo la Kibaha Vijijini kulikuwa na wagombea watatu akiwemo Aliyekuwa akitetea nafasi ya Jimbo hilo Michael Mwakamo, Hamoud Jumaa na Heri Paulo lakini hatahivyo Hamoud ameibuka mshindi.
Katika uchaguzi huo Mramba amesema kuwa Kibaha Vijijini kuna wajumbe wa mkutano Mkuu ambao ni wapiga kura 6,215 lakini katika mkutano huo waliopiga kura ni 5300,zilizoharibika 83 na zilizokataliwa hakuna huku kura halali ni halali ni 5,227 .
Mramba amesema mgombea Heri Paulo amejikuta akipata kura 176 sawa na asilimia 3.37 na Michael Mwakamo akipata kura 1,802 sawa na asilimia 34.46 huku Hamoud Jumaa akijizolea kura 3,247 sawa na asilimia 62.12.
Amesema kwa matokeo hayo amemtangaza Hamoud Jumaa kuwa ndiye mgombea aliyeongoza katika Jimbo la Kibaha Vijijini kwa kunyakua kura nyingi na kuwaacha wenzake mbali.
Jumaa anayejulikana kwa jina maarufu la mzee wa Sambusa aliwai kuwa Mbunge wa Jimbo la Kibaha Vijijini kwa vipindi viwili mfululizo ikiwa kuanzia mwaka 2010 hadi 2020 .
Baaadhi ya Wananchi wa Kibaha wakionyesha bango la kumtaka Hamoud Jumaa kuwa mbunge wa Jimbo la Kibaha Vijijini.
Hatahivyo,Jumaa amewashukuru wajumbe wa mkutano mkuu wa Jimbo la Kibaha Vijijini kwa kumpa heshima ya kumpigia kura nyingi zilizopelekea kuongoza katika uchaguzi huo.
Comments
Post a Comment