RAIS SAMIA ATOA SIKU TANO KWA MAMLAKA YA USIMAMIZI WA BANDARI KUHAMISHIA HUDUMA BANDARI KAVU YA KWALA.

Na Gustaphu Haule,Pwani RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan ametoa siku tano kwa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) kuhakikisha inapeleka huduma zote muhimu katika Bandari Kavu ya Kwala ili kurahisisha huduma kwa watumiaji wa Bandari hiyo. Aidha, Rais Samia ameielekeza Wizara ya Uchukuzi kuhakikisha inashirikiana na sekta binafsi kuhamasisha utumiaji wa miund ombinu ya Bandari Kavu ya Kwala ili kuondoa msongamano wa malori Jijini Dar es Salaam. Rais Samia ametoa maelekezo hayo Julai 31,2025 wakati akizungumza na Wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika Kwala Mkoani Pwani mara baada ya kuzindua Bandari Kavu ya Kwala pamoja na kupokea Mabehewa mapya na yaliyokarabatiwa ya MGR. Amesema, kupatikana kwa huduma hizo katika Bandari Kavu ya Kwala itawasaidia wale wanaohitaji huduma hizo wanapofika Vigwaza wanaingia moja kwa moja Kwala na hivyo kuwaondolea usumbufu madereva kwenda Dar es Salaam. "Kutokana na mahitaji muh...