MBUNGE DR .ALICE KAIJAGE AKABIDHI MITUNGI YA GESI 200 KWA WAFANYAKAZI WA AJIRA MPYA PWANI


Na Gustaphu Haule,Pwani

MBUNGE wa viti maalum kupitia wafanyakazi Dr .Alice Kaijage amekabidhi jumla ya mitungi ya gesi ya  Oryx  200 kwa ajili ya kuwawezesha wafanyakazi wa Mkoa wa Pwani waliopo katika ajira mpya.


Dr.Kaijage amekabidhi mitungi hiyo leo Mei 22, 2025 kwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Pwani Rashid Mchatta hafla ambayo imefanyika katika jengo la ofisi ya Mkuu wa mkoa Pwani .

Awali akizungumza kabla ya kukabidhi mitungi hiyo Dr.Kaijage amesema kuwa amefanya hivyo kwa ajili ya kumuunga mkono Rais wa awamu ya Sita Dr.Samia Suluhu Hassan ambaye ndiye kinara wa Nishati Safi Duniani,Afrika na Tanzania.

"Nimekuja kumuunga mkono Rais Samia kwa suala nzima la Nishati Safi na hizi gesi katoa yeye na mimi nimwakilishi wake kwa upande wa wafanyakazi ambapo lengo kubwa ni kuhakikisha kampeni ya  matumizi ya Nishati Safi inawafikia watu wote," amesema Kaijage.

Aidha, Dr Kaijage amesema kuwa amekabidhi mitungi ya gesi hiyo akiwahamasisha watumishi wa mikoa mbalimbali hapa nchini ukiwemo Mkoa wa Pwani kutumia Nishati Safi ya kupikia ili kumuunga mkono Rais Dr.Samia Suluhu Hassan .

Mbunge wa Vitimaalum kupitia wafanyakazi Dr.Alice Kaijage ( wa pili kutoka kulia) akimkabidhi Katibu Tawala wa Mkoa wa Pwani Rashid Mchatta (kushoto)mitungi ya gesi 200 kwa ajili ya wafanyakazi wa ajira mpya,hafla hiyo imefanyika leo Mei 22,2025 katika jengo la Mkuu wa mkoa wa Pwani

Mbunge Kaijage amesema kuwa mitungi hiyo 200 itagawanywa katika Halmashauri zote tisa za Mkoa wa Pwani hususani kwa watumishi wa ajira mpya ambao wanafanyakazi pembezoni ya Miji kazi ambayo itafanywa na ofisi ya mkuu wa Mkoa wa Pwani kupitia Katibu Tawala.

Amesema kuwa, Rais Samia anapenda kuona wafanyakazi wake wapo katika mazingira mazuri na kwamba licha ya kuboresha mambo mengi mazuri lakini pia anapenda kuona wakati wote wanakuwa na afya njema ya kuweza kulitumikia Taifa.

"Rais wetu mama Samia Suluhu Hassan anapenda kuona watumishi wote wanakuwa na afya njema muda wote na kwakutambua hilo ameona atoe mitungi ya gesi kwa watumishi hasa wa ajira mpya ili waondokane na matumizi ya Kuni na mkaa ," amesema 

Amesema, matumizi ya Kuni na Mkaa yanamadhara makubwa kwani yanasababisha watumishi kuugua magonjwa ya ,kifua, TB sambamba na kuharibu mazingira yanayopelekea kuwepo kwa mabadiliko ya tabia ya nchi( Climate Change).


 Kaijage amesema kuwa Rais Samia anataka watumishi na Watanzania kutumia Nishati Safi ya kupikia kwa ajili ya kutunza mazingira huku akiamini kufanya hivyo itawasaidia watumishi kufanyakazi katika mazingira mazuri na hivyo kuondokana athari za magonjwa yanayotokana na matumizi ya Mkaa na Kuni.

Hatahivyo, mbali na Katibu Tawala kupokea mitungi hiyo lakini pia hafla hiyo ilihudhuriwa na Mkuu wa mkoa wa Pwani Abubakar Kunenge,Wakurugenzi wa Halmashauri pamoja na watumishi mbalimbali.

Mbunge wa Vitimaalum kupitia wafanyakazi Dr. Alice Kaijage  wa pili kutoka kulia akizungumza jambo na Mkuu wa mkoa wa Pwani Abubakar Kunenge mwenye koti la kijivu katika hafla ya kukabidhi mitungi ya gesi 200 kwa ajili ya wafanyakazi wa ajira mpya.



Club News Editor

Comments

Popular posts from this blog

RC PWANI AONGOZA WAKAZI PWANI KUJIANDIKISHA KWENYE DAFTARI LA WAPIGA KURA

BARAZA LA MADIWANI KIBAHA MJINI LAMPONGEZA MKURUGENZI WAKE KWA KAZI NZURI ANAYOIFANYA SAMBAMBA NA KUONGEZA MAPATO.

RAIS SAMIA ATANGAZA KIBAHA MJINI KUWA MANISAPAA,MBUNGE KOKA AFURAHIA ASEMA KIBAHA ITANG'AA