TAKUKURU PWANI YAOKOA ZAIDI YA SH. MILIONI 385 ZA KIJIJI CHA MSUFINI MKURANGA.
Na Gustaphu Haule,Pwani TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Pwani imefanikiwa kuokoa zaidi ya Sh.milioni 385 zilizopotea kupitia akaunti feki ya Kijiji cha Msufini Kidete Wilayani Mkuranga Mkoani Pwani Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Pwani Domina Mukama, ametoa taarifa hiyo leo Mei 29, 2025 katika mkutano wake na Waandishi wa habari ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa majukumu yake katika kipindi cha Januari- Machi 2025. Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Pwani Domina Mukama akizungumza na Waandishi wa habari Mei 29,2025 Mjini Kibaha ikiwa sehemu ya utekelezaji wa majukumu yake katika kipindi cha Januari-Machi 2025 Mukama, amesema kuwa katika kipindi hicho Takukuru Mkoa wa Pwani ilifanya uzuiaji wa vitendo vya rushwa ambapo moja ya vitendo hivyo ni kufanikiwa kuokoa mapato ya asilimia 10 ya mauzo ya ardhi ya Halmashauri ya Kijiji cha Msufini Kidete Wilayani Mkuranga. Mukama, amesema kuwa fedha hizo ambazo ziliwekwa kwenye akaunti feki ya Kijiji hicho iliyogh...