TANZANIA KUSHIRIKIANA NA ITALIA KUENDELEZA SEKTA YA MADINI
Na Gustaphu Haule, Tanzania
#KAZIINAONGEA
SERIKALI ya awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, itaendelea kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia na nchi ya Italia katika kuendeleza Sekta ya Madini nchini hususani katika Teknolojia na mitambo.
Waziri wa Madini Anthony Mavunde, amesena hayo Januari 06, 2025 alipokutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Italia nchini, Giuseppe Coppola, katika ofisi ndogo za Wizara ya Madini Jijini Dar es Salaam.
Balozi wa Italia Nchini Tanzania Giuseppe Coppola (kushoto) akizungumza na Waziri wa Madini Anthony Mavunde(Kulia) Januari 6, katika ofisi za Waziri huyo zilizopo Jijini Dar es Salaam
"Rais wetu Dkt. Samia Suluhu Hassan ameifungua nchi yetu kwa kuimarisha mahusiano Kimataifa kupitia falsafa yake ya 4R, sisi wasaidizi wake tutaendelea kuhakikisha tunasimamia maono hayo na kujenga mahusiano zaidi na washirika wetu kwa manufaa ya uchumi na wananchi wa pande zote", amesema Mavunde
Waziri wa Madini Anthony Mavunde akiwa katika ofisi ndogo za Wizara hiyo zilizopo Jijini Dar es Salaam katika mazungumzo na Balozi wa Italia Nchini Tanzania yaliyofanyika Januari 6,2025.
Mavunde, amesema kuwa zipo fursa nyingi kwenye Sekta ya Madini nchini kuanzia kwenye utafiti mpaka uongezaji thamani madini, mazingira ya uwekezaji ni mazuri hivyo anawakaribisha sana wawekezaji kutoka nchini Italia kuja kuwekeza Tanzania.
Kwa upande wake Balozi Coppola, ameishukuru Serikali ya Tanzania kwa ushirikiano inayompa tangu awasili nchini na kusisitiza kwamba Italia inayo kampuni nyingi ambazo zimejikita katika Teknolojia hususani utengenezaji wa mitambo inayotumika kwenye sekta ya madini.
Balozi wa Italia Nchini Tanzania Giuseppe Coppola akiwa katika ofisi ndogo ya Wizara ya Madini iliyopo Jijini Dar es salaam kwa ajili ya kufanya mazungumzo na Waziri wa Madini Anthony Mavunde yaliyofanyika Januari 6,2025.
"Mwezi Februari, 2025 tunataraji kuwa na mkutano wa wafanyabiashara baina ya Tanzania na Italia ambapo tunatarajia kampuni na wawekezaji katika sekta zote hususan madini kuja kushiriki mkutano huo", amesema Coppola
Amesema kuwa,katika mkutano huo Kampuni za utengenezaji vifaa vya Madini kutoka Italia yatashiriki na Wachimbaji watanufaika na Teknolojia na mitambo rafiki kwa mazingira.
“Ninaamini kwa kutumia mkutano huo utakuwa ni mwanzo mzuri wa wawekezaji kutoka Italia kuona fursa zilizopo nchini Tanzania na kuanza kuzichangamkia" amesisitiza Balozi Coppola.
Waziri Mavunde ameonesha kufurahishwa na mpango wa mkutano wa wafanyabiashara wa Italia na Tanzania, na kusema kwamba ni vizuri taarifa za kina kuhusu mkutano huo zikaifikia Wizara mapema, kwa ajili ya uratibu ili wachimbaji wakubwa na wadogo waweze kushiriki kikamilifu na kuleta tija.
*#KAZIINAONGEA*



.jpg)
Comments
Post a Comment