WAZIRI JAFO AIPIGIA DEBE KAMPUNI YA KINGLION, ATAKA WATANZANIA KUNUNUA BIDHAA ZAO
Na Gustaphu Haule,Pwani
WAZIRI wa Viwanda na Biashara Dk. Selemani Jafo , ametembelea banda la kampuni ya Kinglion lililopo katika Maonesho ya Viwanda ,Biashara na Uwekezaji yanayofanyika katika viwanja vya stendi ya zamani huku akishauri Watanzania kununua bidhaa zinazozalishwa na kampuni hiyo.
Jafo, ametembelea banda hilo leo Disemba 17,2024 akiambatana na viongozi mbalimbali wa Mkoa wa Pwani akiwemo Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakar Kunenge ambapo hatahivyo amepongeza juhudi za uzalishaji zinazofanywa na kampuni ya Kinglion.
Akiwa katika Banda hilo Jafo ameelezwa kuwa kampuni ya Kinglion inazalisha bidhaa mbalimbali ikiwemo Vyombo vya usafiri na usafirishaji kama vile Pikipiki,Mabati,Guta na bidhaa nyingine ambapo amesema Tanzania inapiga hatua kwa kuzalisha bidhaa zake .
"Nawaomba Watanzania kununua bidhaa za Kinglion kwakuwa zina ubora mzuri na imara na tujenge tabia ya kutumia vyakwetu kwakuwa tumefika mahali ambapo tunaweza kuzalisha kila kitu bila kuagiza nje,"amesema Jafo.
Mkuu wa Mkoa wa Pwani ameishukuru kampuni ya Kinglion kwa kuendelea kuwa wadhamini wa maonyesho huku akiahidi suala la kikwazo cha barabara kwenye eneo lao la uwekezaji kushughulikiwa Ili liweze kupitika vizuri muda wote.
Meneja wa Kampuni ya Kinglion Arnold Lyimo ameshukuru kuwepo wa maonesho hayo ambayo yanawapa fursa ya kuonyesha bidhaa zao wanazozalisha.
Lyimo amesema kiwanda cha kuzalisha malighafi za kutengeneza mabati tayari kimejengwa katika eneo la viwanda Zegereni na kinatarajia kuanza kazi mwishoni mwa mwaka huu.
Meneja huyo ameeleza kwamba kiwanda hicho kikianza kufanya kazi kitakuwa kinazalisha tani elfu 35 na kwamba ajira za moja kwa moja 1,500 zitapatikana huku ajira za muda zikikadiriwa kuwa zaidi ya 5000 .
Mwisho
Club News Editor


Comments
Post a Comment