SERIKALI YAPUNGUZA UGUMU WA MAISHA KWA KUSHUSHA BEI YA MAFUTA



Na Gustaphu Haule, Tanzania 

KAZIINAONGEA

RAIS wa awamu ya Sita Dkt. Samia Suluhu Hassan, amefanya juhudi kubwa kwa  kushirikiana na wasaidizi wake katika kuleta unafuu wa maisha ya Mtanzania ikiwa ni kwa kuboresha huduma mbalimbali za kijamii ikiwemo upatikanaji wa Maji, Nishati ya Umeme, Miundombinu ya Barabara, huduma bora za afya, elimu pamoja na huduma nyingine muhimu.

Mbali na kuboresha huduma hizo lakini pia, Rais Samia aliona ni vyema akawapunguzia Watanzania ugumu wa maisha kwa kushusha bei ya mafuta ambayo ni miongoni mwa huduma muhimu katika uzalishaji na ukuaji wa Uchumi. Kupanda kwa gharama za mafuta kunachangia ongezeko la bei za vyakula pamoja na kupanda kwa gharama za usafiri na usafirishaji.

Katika kuliangalia hilo na umuhimu wake, Rais Samia amefanya jitihada katika upatikanaji wa mafuta ya Petroli, Dizeli, na Mafuta ya taa kwa bei nafuu, ili kupunguza mzigo wa gharama za maisha kwa wananchi na kuchochea ukuaji wa Uchumi. 

Katika kukabiliana na hilo, Serikali ilirekebisha na kuimarisha mfumo wa ununuzi wa mafuta kwa pamoja  "Bulk Procurement System" (BPS). Mfumo huu unawezesha ununuzi wa mafuta kwa wingi moja kwa moja kutoka kwa wazalishaji wakuu, hivyo kupunguza gharama za uagizaji na kuhakikisha bei zinazofikiwa zinakuwa nafuu kwa watumiaji.


Pia Serikali ilifanya juhudi za makusudi ambapo kuanzia Oktoba 5, 2021, Serikali ilipunguza tozo mbalimbali za Taasisi zake kwa kiwango cha Shilingi 29.38 kwa lita ya Petroli, Shilingi 30.05 kwa lita ya Dizeli na Shilingi 26.99 kwa lita ya Mafuta ya taa.



Mbali ya hilo pia Serikali imeimarisha miundombinu ya kuhifadhi mafuta (Strategic Reserves), hatua inayowezesha upatikanaji wa mafuta hata wakati wa upungufu wa Kimataifa au majanga ya dharura lakini pia imeimarisha na kuboresha Uwekezaji katika usambazaji wa mafuta.


Mafanikio haya ya Serikali ya Rais Samia, katika kipindi cha miaka mitatu yaliendelea kuonekana ambapo jitihada zaidi zilifanyika katika kushusha gharama za maisha ambapo Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), ilitangaza bei kikomo za bidhaa za mafuta ya Petroli hapa nchini ambapo katika Disemba 2022 bei ya mafuta ya rejareja ya Petroli kwa Dar es Salaam na Mtwara zilipungua kwa Shilingi 59/lita na 92/lita, mtawalia, ikilinganishwa na bei za Novemba 2022, wakati bei ya Tanga imeongezeka kwa Shilingi 9/lita.

Hata hivyo, ili kuendelea kupunguza athari za ongezeko la bei za mafuta nchini ambapo shughuli nyingi za kiuchumi zinategemea Dizeli, Serikali ilitoa ruzuku kwa bei za Disemba 2022 ambapo kutokana na ruzuku hiyo, bei ya mafuta ya Dizeli ilipungua kwa Shilingi 83/lita, Shilingi 247/lita na Shilingi 243/lita kwa Dar es Salaam, Tanga na Mtwara, mtawalia.



Kwa mwezi Disemba, 2023 bei za mafuta (FOB) kwenye Soko la Dunia zilipungua kwa wastani
wa asilimia 0.86 kwa mafuta ya Petroli na asilimia 9.11 kwa mafuta ya Dizeli na gharama za kuagiza mafuta (Premium) kwa Bandari ya DSM zilipungua kwa wastani wa asilimia 24 kwa mafuta ya Petroli na asilimia 30 kwa mafuta ya Dizeli.

Kwa Bandari ya Tanga gharama za kuagiza mafuta (Premium) zilipungua kwa asilimia 30 kwa mafuta ya Petroli na asilimia 17 kwa mafuta ya Dizeli.

Bandari ya Mtwara haikupokea shehena ya mafuta ambapo mabadiliko ya bei za mafuta kwa mwezi Disemba 2023 yanatokana na kupungua kwa bei za mafuta ghafi katika Soko la Dunia kwa wastani wa asilimia 8.72 na gharama za uagizaji wa mafuta kwa wastani wa asilimia 27 kwa Petroli na asilimia 

Bidhaa za mafuta zinazoagizwa na kupokelewa hapa nchini zinazingatia bei za mafuta yaliyosafishwa (FOB) kutoka soko la Uarabuni ambapo mwezi Disemba 2024, bei kikomo za mafuta zimekokotolewa kwa kuzingatia bei za soko la Uarabuni za mwezi Novemba 2024, ikilinganishwa na Mwezi Oktoba 2024, bei za mwezi Novemba zimepungua kwa asilimia 0.29 kwa mafuta ya Petroli, kuongezeka kwa asilimia 2.11 kwa mafuta ya Dizeli na asilimia 2.28 kwa mafuta ya taa.

Gharama za uagizaji mafuta (Premiums) zimeongezeka kwa wastani wa asilimia 7.26 kwa Petroli na kupungua kwa asilimia 12.80 kwa dizeli na wastani wa asilimia 7.10 kwa mafuta ya taa katika Bandari ya Dar es Salaam hakuna mabadiliko katika Bandari ya Tanga na zimeongezeka kwa wastani wa asilimia 15.67 kwa mafuta ya Petroli na hakuna mabadiliko kwa mafuta ya Dizeli katika Bandari ya Mtwara.

MWENENDO WA GHARAMA ZA UAGIZAJI

Gharama za uagizaji mafuta (Premiums) zimeongezeka kwa wastani wa asilimia 7.26 kwa Petroli na kupungua kwa asilimia 12.80 kwa Dizeli na wastani wa asilimia 7.10 kwa mafuta ya taa katika Bandari ya Dar es Salaam, hakuna mabadiliko .

Katika Bandari ya Tanga gharama zimeongezeka kwa wastani wa asilimia 15.67 kwa mafuta ya petroli na hakuna mabadiliko kwa mafuta ya dizeli katika Bandari ya Mtwara.

Jitihada hizi zilizofanywa na Serikali zimesaidia kwa kiasi kikubwa kupungua kwa gharama za mafuta na hivyo kurahisisha maisha ya Watanzania.

*#KAZIINAONGEA*



Club News Editor - Charles Kusaga

Comments

Popular posts from this blog

RC PWANI AONGOZA WAKAZI PWANI KUJIANDIKISHA KWENYE DAFTARI LA WAPIGA KURA

BARAZA LA MADIWANI KIBAHA MJINI LAMPONGEZA MKURUGENZI WAKE KWA KAZI NZURI ANAYOIFANYA SAMBAMBA NA KUONGEZA MAPATO.

RAIS SAMIA ATANGAZA KIBAHA MJINI KUWA MANISAPAA,MBUNGE KOKA AFURAHIA ASEMA KIBAHA ITANG'AA