SERIKALI YA AWAMU YA SITA YAENDELEA NA MABORESHO YA MIFUMO YA UTOAJI HAKI


Na Gustaphu Haule, Tanzania 

#KAZIINAONGEA

SERIKALI ya awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, imeendelea kufanya maboresho na mapitio ya mifumo ya utoaji haki yenye lengo la kuimarisha ukuaji kiuchumi na kijamii.

Matokeo haya ni miongoni mwa jitihada zinazofanywa na Rais Samia katika utawala wake kwa kipindi cha miaka mitatu akiwa na lengo la kuleta usawa kwa Watanzania na kuinua uchumi wa Taifa kwa ujumla.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameongea hayo Disemba 03, 2024, alipomwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Mkutano wa 21 wa Chama cha Majaji na Mahakimu wa Afrika Mashariki uliofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Hotel ya Gran Melia Jijini Arusha.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza alipofungua Mkutano wa 21 wa Chama cha Majaji na Mahakimu wa Afrika ya Mashariki  kwenye ukumbi wa hoteli ya GranMelia jijini Arusha, Desemba 3, 2024. Mheshimiwa Majaliwa alimwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwenye ufunguzi huo.

Amewaeleza Majaji na Mahakimu hao kuwa, Serikali chini ya uongozi wa Rais Dkt. Samia, imefanya maamuzi muhimu ya kisera, kijamii na kiuchumi ambayo yanaakisi mwelekeo wa maendeleo wenye lengo la kuboresha ustawi wa watu wa Tanzania.

Kupitia Mpango wa Maendeleo ya Miaka Mitano, Serikali ya Tanzania imedhihirisha dhamira yake ya kuboresha mfumo wa utoaji haki ambapo mnamo mwaka 2023, Rais Samia aliteua "Tume ya Rais ya Haki Jinai" yenye lengo la kuleta mageuzi katika mfumo wa haki za jinai.

Waziri Mkuu amewataka Majaji na Mahakimu hao kujadili namna mifumo ya utoaji haki, inavyoweza kusaidia katika kukuza mtangamano wa kikanda na ukuaji wa uchumi.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimsikiliza Mtendaji Mkuu wa Mahakama  Tanzania, Profesa Elisante Ole Gariel alipotoa maelezo mafupi kabla ya Waziri Mkuu kufungua mkutano wa 21 wa Chama cha Majaji na Mahakimu wa Afrika ya Mashariki kwenye ukumbi wa hoteli ya GranMelia jijini Arusha, Desemba  3, 2024. Mheshimiwa Majaliwa alimwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwenye ufunguzi huo. 

Ametoa wito kwa Chama cha Majaji na Mahakimu wa Afrika Mashariki kuendelea kujadili changamoto katika utoaji haki na kuweka mipango endelevu ya namna ya kukabiliana na changamoto hizo kupitia mikutano yake.

"Mkutano huu pamoja na mambo mengine ni muhimu kujadili masuala muhimu ya Kitaifa na Kikanda katika mfumo wa utoaji haki, pia nina imani kupitia mkutano huu mtajadili umuhimu wa kuimarisha na kuboresha mifumo ya utoaji haki na kutumia ukuaji wa teknolojia ili kuboresha kwenye ufanisi wa majukumu yenu," amesema Waziri Mkuu

*#KAZIINAONGEA*


Club News Editor - Charles Kusaga

Comments

Popular posts from this blog

RC PWANI AONGOZA WAKAZI PWANI KUJIANDIKISHA KWENYE DAFTARI LA WAPIGA KURA

BARAZA LA MADIWANI KIBAHA MJINI LAMPONGEZA MKURUGENZI WAKE KWA KAZI NZURI ANAYOIFANYA SAMBAMBA NA KUONGEZA MAPATO.

RAIS SAMIA ATANGAZA KIBAHA MJINI KUWA MANISAPAA,MBUNGE KOKA AFURAHIA ASEMA KIBAHA ITANG'AA