SERIKALI IMEENDELEA KUBORESHA NA KUWEKA MAZINGIRA WEZESHI KWA VIJANA



Na. Julieth Ngarabali

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Ridhiwani Kikwete amesema Serikali imejidhatiti kuweka mazingira yanayowezesha vijana kutoka kwenye uchumi usio rasmi kuelekea uchumi ulio rasmi.


“Serikali inaendelea kuimarisha sera zinazowezesha nguvu kazi ya taifa, kuondoa vikwazo vya Kibiurokrasi, kutoa msaada wa kiufundi  na kifedha kwa Vijana” amesema.

Mhe. Ridhiwani amebainisha hayo Novemba 29, 2024 Jijini Dar es salaam, wakati wa uzinduzi wa uchambuzi wa kina wa sekta isiyo rasmi katika biashara zinazoongozwa na Vijana.


Aidha, amesema tafiti zilizofanywa sekta zisizo rasmi zitasaidia kupata majawabu ya matatizo ya Vijana katika kukabiliana na changamoto isiyo rasmi.

Uzinduzi huo umehudhuriwa na Mkurugenzi  wa Shirikia la Kazi Duniani Kanda ya Afrika Mashariki Bi. Caroline Mugalla, Mkurugenzi Mtendaji na Afisa Mtendaji Mkuu wa ATE Bi. Suzanne Ndomba na Watafiti Mashuhuri.





Club News Editor

Comments

Popular posts from this blog

BARAZA LA MADIWANI KIBAHA MJINI LAMPONGEZA MKURUGENZI WAKE KWA KAZI NZURI ANAYOIFANYA SAMBAMBA NA KUONGEZA MAPATO.

RAIS SAMIA ATANGAZA KIBAHA MJINI KUWA MANISAPAA,MBUNGE KOKA AFURAHIA ASEMA KIBAHA ITANG'AA

RC PWANI AFURAHISHWA NA UTENDAJI KAZI WA MKURUGENZI WA KIBAHA MJINI DKT.ROGERS SHEMWELEKWA