RC ANDENGENYE AMSHUKURU RAIS SAMIA KUUFUNGUA MKOA WA KIGOMA KIUCHUMI


Na Gustaphu Haule,Tanzania

#KAZIINAONGEA
 
DISEMBA 5, 2024 ilikuwa  ni siku ya aina yake, ambayo haijawahi kutokea kwa historia ya matukio ya uwanja wa 
Kawawa na ya elimu katika mji wa Kigoma Ujiji.

Ilikuwa kama hadithi lakini sasa ni vitendo halisi vinavyotekelezwa  na  Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan katika upande wa sekta ya elimu nchini.

Mahafali ya kihistoria ya Chuo Kikuu Huria cha Tanzania ambayo yamewakusanya wahitimu wa Chuo hicho kutoka mikoa yote ya Tanzania yamefanyika hapo na mgeni rasmi alikuwa ni Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Majaliwa aliyemwakilisha Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango.

  


Kufanyika kwa mahafali hayo katika manispaa ya Kigoma Ujiji ni ishara ya utekelezaji wa juhudi kubwa za Dkt.Samia za kuzidi kuufungua mkoa wa Kigoma Kiuchumi na kuongeza fursa za elimu kwa wananchi wa mkoa huo na maeneo ya jirani.

Aidha, katika eneo la Chuo hicho kilichopo kata ya Kasimbu Ujiji jirani ya Shule ya Sekondari Kasingirima, Mkuu wa mkoa wa Kigoma Thobias Andengenye aliushukuru uongozi na baraza la Chuo kwa uamuzi huo wa kufanya mahafali yao ya 43  katika mkoa wa Kigoma.

Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Thobias Andengenye akihutubia wakati wa mahafali ya 43 ya Chuo kikuu huria cha Tanzania

"Kigoma ni pahali sahihi na patulivu na kuna chakula cha kutosha hivyo maamuzi yaliyofanyika kuleta mahafali haya kwetu ni jambo jema lenye kuleta heshima hapa Mkoani kwetu, "amesema Andengenye.

Mkutano huo ulihudhuriwa na katibu mkuu wa wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof.Caroline Nombo, Maprofesa, madaktari waandamizi na wanataaluma.

Katika hatua nyingine mtoa mada mkuu, Prof.Yunus Mgaya na wajadili mada walieleza kuwa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania kimekuwa na mchango mkubwa katika kufungua fursa za watu wa Kigoma na maeneo mengine katika kupata elimu.

Katika hotuba yake Andengenye amemshukuru Rais Samia kwa juhudi zake za kuifungua Kigoma kiuchumi na pia amewataka wananchi kuwa na utayari wa kujiunga na chuo hicho.

*#KAZIINAONGEA*
Club News Editor

Comments

Popular posts from this blog

RC PWANI AONGOZA WAKAZI PWANI KUJIANDIKISHA KWENYE DAFTARI LA WAPIGA KURA

BARAZA LA MADIWANI KIBAHA MJINI LAMPONGEZA MKURUGENZI WAKE KWA KAZI NZURI ANAYOIFANYA SAMBAMBA NA KUONGEZA MAPATO.

RAIS SAMIA ATANGAZA KIBAHA MJINI KUWA MANISAPAA,MBUNGE KOKA AFURAHIA ASEMA KIBAHA ITANG'AA