MIAKA 63 YA UHURU WA TANGANYIKA NA AJIRA 37,473 ZA WALIMU
Na Gustaphu Haule,Tanzania
#KAZIINAONGEA
KATIKA kuadhimisha miaka 63 ya Uhuru wa Tanganyika Serikali ya awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, katika kipindi cha kuanzia Mwezi Machi 2021 hadi Oktoba 2024 jumla ya walimu 37,473 wameajiriwa na kupangiwa vituo vya kazi katika Mamlaka za Serikali za Mitaa.
Utaratibu unaofanywa na Serikali katika usajili wa Walimu ni kwamba, Tume ya Utumishi wa Walimu inasajili walimu wanaofundisha Shule za Msingi na Sekondari mara baada ya kuajiriwa katika Utumishi wa Umma.
Awali katika kipindi cha kuanzia mwezi Machi 2021 hadi Mwezi Machi 2022 idadi ya Walimu 6,963 walisajiliwa, katika idadi hiyo walimu 4,044 ni wa Shule za Msingi na walimu 2, 919 ni wa Shule za Sekondari.
Kufuatia agizo la Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alilolitoa katika sherehe za Siku ya Wafanyakazi 1 Mei, 2021, kuwa Watumishi wa Umma wenye sifa za kupanda vyeo wapandishwe.
TSC ilipandisha vyeo Walimu 126,346 wa Shule za Msingi na Sekondari, idadi hii ni imejumuisha lkama ya miaka mitatu mfululizo yaani 2018/2019, 2019/2020 na 2020/2021.
Kutokana na mwongozo uliotolewa na Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora (MUUUB) juu ya namna ya kuendesha zoezi hilo, TSC ilipandisha walimu wote waliokuwa na sifa za kupanda daraja.
*Ongezeko za Shule za Msingi na Sekondari*
Kwa upande wa mafanikio katika kuongeza idadi ya shule hapa nchini, kwa Tanzania Bara kumekuwa na ongezeko la Idadi ya shule za msingi kutoka shule 3,270 mwaka 1961 hadi shule 20,384 mwaka 2024.
Katika ubora kitaaluma, mazingira hata programu zinazotolewa ambapo pia Serikali ya Tanzania imekuwa inatoa ruzuku kwa shule za Sekondari.
Kupitia mradi wa Kuboresha Elimu ya Sekondari (SEQUIP), Serikali imepanga kujenga shule za bweni za wavulana za Kitaifa saba, zitakazochukua wanafunzi 1,080 kwa kila moja.
Serikali imehakikisha kuwa, shule za kidato cha tano na sita zinapata miundombinu muhimu ikiwemo mabweni ili wanafunzi wanaomaliza kidato cha nne na kufaulu wanapata nafasi.
*Kiwango cha ufaulu*
Kwa upande wa matokea ya upimaji wa Kitaifa wa darasa la Nne, Jumla ya Wanafunzi 1,287,934 kati ya 1,545,330 sawa na asilimia 83.34 wamefaulu kwa kupata madaraja ya A, B, C na D.
Kumekuwa na ongezeko la ufaulu kwa asilimia 0.39 kwa Wanafunzi wanaoendelea na darasa la Tano ikilinganishwa na mwaka 2022
Kwa mujibu wa Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA), Januari 07, 2024 lilitangaza matokeo ya Mtihani upimaji wa Kitaifa Kidato cha Pili ambapo Jumla ya Wanafunzi 592,741 kati ya 694,769 wamefaulu sawa na asilimia 85.31.
Kiwango hicho cha ufaulu kimeongezeka kwa asilimia 0.13 ikilinganishwa na asilimia 85.18 ya Wanafunzi waliofaulu Mtihani huo mwaka jana.
*#KAZIINAONGEA*
Comments
Post a Comment