DC MANGOSONGO AMSHUKURU RAIS SAMIA KUMNUNULIA GARI JIPYA LA KAZI.RC KUNENGE ASISITIZA KUCHAPAKAZI
Na Gustaphu Haule,Pwani
MKuu wa Wilaya ya Mafia Aziza Mangosongo amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt .Samia Suluhu Hassan kwa jitihada ya kuiwezesha ofisi yake kupata gari mpya la kisasa.
Mangosongo ametoa shukrani hizo mara baada ya kukabidhiwa gari mpya kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakar Kunenge katika hafla ambayo imefanyika Disemba 4,2024 katika viwanja vya ofisi ya Mkuu wa Mkoa Pwani iliyopo Mjini Kibaha.
Katika hafla hiyo Mangosongo pamoja na wakuu wa Wilaya wengine watatu walikabidhiwa magari hayo ikiwa ni awamu ya pili ya Wakuu wa Wilaya wa Mkoa wa Pwani kupewa magari kwani kwa awamu ya kwanza Wilaya mbili zilipata magari hayo .
Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakar Kunenge akiwa tayari kukata utepe Kwa ajili ya hafla ya kukabidhi magari manne ya Wakuu wa Wilaya ,hafla hiyo imefanyika Disemba 4 Mjini Kibaha
"Ninamshukuru Rais Samia kwa kuweza kuninunulia gari hili, mimi kama Mkuu wa Wilaya gari hili linaenda kuongeza utendaji kazi katika kuwatumikia Wananchi kwa kuwatatulia kero zao na hata kuzipatia ufumbuzi changamoto zinazowakabili," amesema Mangosongo
Amesema,gari hilo ni kitendeakazi kikubwa ambacho kitamsaidia kufanyakazi usiku na mchana na kufika mahali popote kwa urahisi na kusema kwasasa hakuna kisingizio.
"Kilio cha usafiri kilikuwa kikubwa lakini Rais Dkt .Samia ni mchapakazi na anatekeleza kwa vitendo ndio maana leo hii amekuwa akitujali Wakuu wa Wilaya kwa kutununulia magari mapya ya kisasa," amesema Mangosongo
Mangosongo, amesema kwakuwa anakwenda kufanyakazi kwa bidii na kulitumia gari hilo kikamilifu na kuhakikisha analitunza ili liweze kufanyakazi iliyokusudiwa.
Nae Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakar Kunenge,amemshukuru Rais Samia kwakuwa ndani ya mwaka mmoja tayari Wilaya Sita zimepata magari mapya.
Kunenge,amesema miezi mitatu iliyopita Wilaya ya Kisarawe na Bagamoyo zilipata magari lakini kwasasa zimepata tena magari manne ambayo yamekwenda Rufiji,Mkuranga,Mafia na Kibaha.
"Mwaka mmoja tumepata magari Saba kwahiyo hakuna sababu ya kushindwa kufanyakazi hivyo lazima tupongeze juhudi za Rais na sasa kinachotakiwa ni kufanyakazi ili kuhakikisha yale anayoyataka Rais Samia tunatekeleza kwa wakati,"ameongeza Kunenge
Hatahivyo, Kunenge amesema licha ya Wilaya hizo kupewa magari hayo lakini hata ofisi ya Mkuu wa Mkoa nayo imepata gari ambapo ameongeza kuwa kazi iliyobaki ni kufanyakazi ili kutimiza matarajio ya Rais
Mwisho.
Comments
Post a Comment