UKWAA LA WAHARIRI LAIPONGEZA SERIKALI YA RAIS SAMIA KWA KUUNDA BODI YA ITHIBATI.



Na Gustaphu Haule,Tanzania

#KAZIINAONGEA

MWENYEKITI wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Deodatus Balile ameimpongeza Serikali ya awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa  kujali maslahi ya Wanahabari nchini ikiwa ni pamoja na kuridhia Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Jerry  Silaa aunde Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari mara baada ya kumteua.

Balile amesema hiyo ni hatua kubwa kwani imechukua miaka nane tangu kutungwa kwa Sheria ya Huduma za Habari Sura ya 229 inayotamka uundwaji wa bodi hiyo.

MWENYEKITI wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Deodatus Balile

Ametoa kauli hiyo  Novemba 21, 2024 wakati akiwasilisha hoja za jukwaa hilo mbele ya Waziri kwenye Kikao cha kwanza cha kufahamiana na Wajumbe wa Umoja wa Haki ya Kupata Taarifa (CoRI) kilichofanyika Ukumbi wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), jijini Dar es Salaam.

“Tunakushukuru sana mheshimiwa kwa sababu imechukua miaka nane tangu Sheria imepita 2016  na Bodi ilikuwa haijawahi kuundwa na leo tumemsikia Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi  Patrick Kipangula siyo mgeni sana kwetu lakini leo tumemsikia kwa cheo kipya tunashukuru sana na tunampongeza sana,” amesema Balile

Waziri Silaa aliiteua  Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari Septemba 18,2024  na kumteua Mwandishi wa Habari Nguli, Tido Mhando kuwa Mwenyekiti wa Kwanza na wajumbe wengine sita kutoka Taasisi za Habari kama ilivyoainishwa katika Sheria ya Huduma za Habari.


Wajumbe wa Bodi hiyo ni pamoja na Thobias Makoba, Mgaya Kingoba, Dkt. Rose Reuben Mchomvu, Dkt Egbert Mkoko na Laslaus Komanya.

Akizungumza na Wadau wa Habari kuelekea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024 na Uchaguzi Mkuu 2025, Novemba 19,2024, Waziri Silaa alibainisha kuwa uzinduzi rasmi wa bodi hiyo muhimu utafanyika mapema mwezi Desemba, 2024 na kwamba itafungua njia ya safari ya kuanzisha Baraza Huru la Habari na pia Mfuko wa Mafunzo kwa Wanahabari na tathimini ya hali ya uchumi kwa vyombo vya habari.

Katika hoja yake Balile alimuomba Waziri kuwa na kikao kazi kitakachogusia Sera ya Habari, Sheria na mfuko wa mafunzo ili kupata uelewa wa pamoja wa namna ya kuiboresha tasnia ya Habari na Uhuru wa Vyombo vya Habari.

Ombi kama hilo pia liliwasilishwa na Mwenyekiti wa CoRI, Ernest Sungura aliyemuomba Waziri katika vikao vijavyo kuwa na majadiliano ya namna Baraza Huru la Habari lililoundwa na Sheria ya Huduma za Habari  litakavyoendesha majukumu yake ili kujitofautisha na Baraza la Habari Tanzania (MCT) na kuondoa mgongano.

# KAZIINAONGEA
Club News Editor - Charles Kusaga

Comments

Popular posts from this blog

RC PWANI AONGOZA WAKAZI PWANI KUJIANDIKISHA KWENYE DAFTARI LA WAPIGA KURA

BARAZA LA MADIWANI KIBAHA MJINI LAMPONGEZA MKURUGENZI WAKE KWA KAZI NZURI ANAYOIFANYA SAMBAMBA NA KUONGEZA MAPATO.

RAIS SAMIA ATANGAZA KIBAHA MJINI KUWA MANISAPAA,MBUNGE KOKA AFURAHIA ASEMA KIBAHA ITANG'AA