SHIRIKA LA OCODE LATOA MAFUNZO KABAMBE YA YA STADI ZA MAISHA WILAYANI BAGAMOYO


NA VICTOR MASANGU,BAGAMOYO 

Shirika lisilokuwa la kiserikali la Organization for Community Development (OCODE) limetoa mafunzo maalumu juu ya stadi za maisha kwa  wazazi,walimu pamoja  na watoto waliopo majumbani kwa lengo la kuweza kukabiliana na changamoto mbali mbali za kimaisha.

Hayo yamebainishwa na mratibu wa stadi za maisha Wilaya ya Bagamoyo kutoka shirika la Ocode  Tunu Sanga wakati wa kutoa  mafunzo hayo ambayo yamefanyika katika shule ya msingi Nianjema.

Mratibu wa Mradi wa Stadi za maisha Wilaya ya Bagamoyo Tunu Sanga akizungumza wakati wa kutoa Mafunzo

Alisema kwamba shughuli hiyo ya kutoa elimu ya stadi za maisha imeweza kuwafikia jumla wa wajumbe wapatao 109 kutoka maeneo mbali mbali ya Wilaya ya Bagamoyo.

Alisema kwamba katika mafunzo hayo pia wameamua kuwashirikisha na viongozi mbali mbali wa dini ambao wataweza kutoa elimu kwa wananchi wengine kuhusians na umuhimu wa stadi za maisha.

"Tumekutana na makundi mbali mbali ikiwemo wazazi,walimu na watoto waliopo majumbani ili kuweza kukaa nao kwa pamoja na kuwapatia namna bora ya kuweza kukuza hizi stadi za maisha hasa kwa wale watoto waliopo majumbani," alisema Tunu.


Kadhalika Tunu alifafanua kwamba wameweza kufundisha namna ya kuweza kujiamini,stadi ya ushirikiano,masuala mbali mbali ya kutatua matatizo,heshima pamoja na mambo ya ubunifu.

Mratibu huyo alifafanua kuwa pia  katika mafunzo pia  yamewajumuisha wajumbe wa kamati za shule mbalimbali, umoja wa walimu (UWAWA) ambao nao wataweza kusaidia katika suala zima la stadi  za maisha.

Naye mgeni rasmi katika mafunzo hayo Afisa elimu maalumu Sekondari Wilaya ya Bagamoyo Frank Kwayu amelipongeza shirika la OCODE kwa kuweza kutoa stadi za maisha ambazo zitakwenda kuwasaidia walimu, wazazi na wanafunzi katika kutatua changamoto zao.

Afisa Elimu huyo alisema kwamba shirika la OCODE limeweza kufanya kitu kizuri kwa kuamua kushirikiana bega kwa bega na serikali ya Wilaya ya Bagamoyo katika suala zima la stadi za maisha na kwamba mafunzo hayo yataweza kuwa chachu ya  maendeleo.

"Tunashukuru sana kwa wenzetu wa shirika la OCODE kwa kuweza kuja Wilayani kwetu na kuweza kutoa mafunzo  juu ya stadi za maisha kwa makundi mbali mbali na sisi tutawapa ushirikiano katika shughuli zao,"alisema Afisa elimu huyo.

Shirika  la OCODE kwa sasa limeshafanikiwa kutoa mafunzo hayo kwa zaidi ya wajumbe wapatao  109  na kuweza kuzifikia shule nne nne za msingi katika kutoa elimu hiyo ikiwemo shule ya Msingi Mataya,Bigilo,Ukuni pamoja na shule ya msingi Nia njema zote za Wilaya ya Bagamoyo.


Club News Editor - Charles Kusaga

Comments

Popular posts from this blog

BARAZA LA MADIWANI KIBAHA MJINI LAMPONGEZA MKURUGENZI WAKE KWA KAZI NZURI ANAYOIFANYA SAMBAMBA NA KUONGEZA MAPATO.

RAIS SAMIA ATANGAZA KIBAHA MJINI KUWA MANISAPAA,MBUNGE KOKA AFURAHIA ASEMA KIBAHA ITANG'AA

RC PWANI AFURAHISHWA NA UTENDAJI KAZI WA MKURUGENZI WA KIBAHA MJINI DKT.ROGERS SHEMWELEKWA