SERIKALI YATUMIA BILIONI 300 KUGHARAMIA MATIBABU YA WAGONJWA WA KISUKARI KWA MWAKA

     

Na Gustaphu Haule, Tanzania 

SERIKALI kupitia mkakati wa tano wa Sekta ya Afya (HSSP V) imetangaza mipango na mikakati madhubuti ya kuzuia na kudhibiti magonjwa yasiyoambukiza, ikiwemo ugonjwa wa kisukari kwa kuimarisha utoaji elimu kwa umma juu ya njia za kujikinga.


Hatua hiyo inalenga kupunguza kasi ya magonjwa hayo ambayo yanaigharimu Serikali ya awamu ya sita, inayoongozwa na Rais. Dkt. Samia Suluhu Hassan, jumla ya Shilingi Bilioni 300 kila mwaka kugharamia matibabu wagonjwa hao.

Kupitia mkakati huo, sekta ya afya imetoa kipaumbele kwa kuweka mikakati madhubuti ya kuzuia na kudhibiti magonjwa yasiyoambukiza ikiwemo kisukari kwa kuimarisha utoaji wa elimu ya Afya kwa umma juu ya kujikinga na ugonjwa huo kama vile kuzingatia ulaji unaofaa, kushughulisha mwili, mazoezi ya viungo pamoja na kuepuka matumizi ya pombe na tumbaku.

Naibu Waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel ameyasema hayo Oktoba 29, 2024 Bungeni Jijini Dodoma wakati akijibu swali la Mbunge wa viti maalum  Mwantumu Dau Haji, aliyetaka kujua Serikali ina mpango gani wa kutatua changamoto ya ugonjwa sugu wa kisukari nchini.


Molel, amesema kuwa sekta ya afya imetoa kipaumbele kwa kuweka mikakati madhubuti ya kuzuia na kudhibiti magonjwa kwa kuendelea kuimarisha upatikanaji wa dawa, vitendanishi na mashine za kupimia sukari kwa maeneo yote ya kutolea huduma za afya.

Katika jitihada hizo za Serikali, pia inaendelea kutoa mafunzo ya kibingwa kwa wataalamu wa afya juu ya matibabu ya ugonjwa wa kisukari ili kuwawezesha kutoa huduma bora kwa wagonjwa wa kisukari.


Mkakati huo unalenga kukuza ufahamu juu ya ulaji bora, kufanya mazoezi, kuepuka matumizi ya pombe na tumbaku, kuwawezesha watoa huduma kutoa huduma bora kwa wagonjwa wa kisukari na kuboresha mapambano dhidi ya kisukari.

#KAZIINAONGEA



Comments

Popular posts from this blog

RC PWANI AONGOZA WAKAZI PWANI KUJIANDIKISHA KWENYE DAFTARI LA WAPIGA KURA

BARAZA LA MADIWANI KIBAHA MJINI LAMPONGEZA MKURUGENZI WAKE KWA KAZI NZURI ANAYOIFANYA SAMBAMBA NA KUONGEZA MAPATO.

RAIS SAMIA ATANGAZA KIBAHA MJINI KUWA MANISAPAA,MBUNGE KOKA AFURAHIA ASEMA KIBAHA ITANG'AA