SERIKALI YATAKA GHARAMA ZA UMEME VIJIJINI IWE SH.27 000 TU, MKURUGENZI TANESCO AAGIZWA KUSIMAMIA KIKAMILIFU



Na Gustaphu Haule, Tanzania 

#KAZI INAONGEA

SERIKALI ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imesisitiza kuwa gharama ya kuweka umeme kwa vijiji vyote nchini ni iwe ni  Sh.27,000 na sio zaidi ya hapo.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Nishati, Judith Kapinga kwa niaba ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko Jijini Dodoma hivi karibuni.


Katika kuhakikisha hilo linatekelezwa, Kapinga alimwagiza Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO,  Mhandisi Gissima Nyamo-Hanga kufanya mapitio ya maeneo ya Vijiji ambayo yanalipishwa bei ya mjini kuunganisha umeme ili waweze kulipa bei stahiki ya Vijiji ambayo ni shilingi 27,000.

Akijibu swali la la Mbunge wa Bukoba Vijijini, Samsung Rweikiza aliyetaka kufahamu Serikali inachukua hatua gani kwa wananchi wa Vijijini wanaolipia gharama ya kuunganisha umeme ya  zaidi ya 27,000.

"Kuna baadhi ya maeneo ya Vijiji yamekuwa yakitozwa gharama ya shilingi 321,000, namuagiza Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO kufanya mapitio ya maeneo haya", Amesisitiza Kapinga

Aidha, kuhusu Serikali kupeleka umeme katika vitongoji visivyokuwa na umeme Bukoba Vijijini, Kapinga amesema Serikali inaendelea kuunganisha vitongoji ambavyo havina umeme ambapo vitongoji 258 kati 515 vya Jimbo la Bukoba Vijijjini vimefikishiwa umeme.

Hivyo, kazi ya kupeleka umeme katika vitongoji 27 ambavyo havina umeme katika Jimbo la Bukoba Vijijini inaendelea kupitia miradi ya ujazilizi 2B na Mradi wa Kupeleka umeme katika Vitongoji awamu ya Pili A (HEP IIA).

Club News Editor - Charles Kusaga

Comments

Popular posts from this blog

RC PWANI AONGOZA WAKAZI PWANI KUJIANDIKISHA KWENYE DAFTARI LA WAPIGA KURA

BARAZA LA MADIWANI KIBAHA MJINI LAMPONGEZA MKURUGENZI WAKE KWA KAZI NZURI ANAYOIFANYA SAMBAMBA NA KUONGEZA MAPATO.

RAIS SAMIA ATANGAZA KIBAHA MJINI KUWA MANISAPAA,MBUNGE KOKA AFURAHIA ASEMA KIBAHA ITANG'AA