SERIKALI KUZIFUNGIA PROGRAMU 69 ZINAZOTOA MIKOPO KIDIGITALI



Na Gustaphu Haule, Tanzania 


*Ni zile zinazotoa mikopo na kusambaza ujumbe wa kudhalilisha wateja*

#KAZIINAONGEA

SERIKALI kupitia Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imetangaza kuzifungia programu Tunisi (Application) 69 ambazo zimekuwa zikitoa mikopo ya Kidigitali bila kuwa na leseni na idhini kutoka Benki Kuu ya Tanzania (BoT).



Hatua hii imekuja kufuatia kuwepo kwa malalamiko kutoka kwa wateja  kusambazwa ujumbe kwa jamaa zao huku wakitukanwa na kudhalilishwa na Programu hizo zinazotoa mikopo kwa njia ya mitandao.

Kufungiwa kwa programu hizi ni miongoni mwa mikakati ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kuzitaka Taasisi za kifedha na Programu Tunisi kufanya shughuli zake za kifedha kwa kufuata taratibu na sheria za mikopo walizowekewa.

Miongoni mwa majukwaa iliyofungiwa ni Jokate Foundation Imarisha Maisha ambalo matapeli walitumia kinyume na utaratibu jina la Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa CCM, Jokate Mwegelo (MNEC) ili kudanganya Umma wa Watanzania na kujipatia kipato kisicho na uhalali wa kisheria

Mwongozo huo uliotolewa na Benki Kuu ya Tanzania (BOT), unalenga kuimarisha usimamizi wa watoa huduma ndogo za fedha daraja la Pili chini na kuhakikisha uzingatiwaji wa kanuni za kumlinda mlaji na huduma za fedha ikijumuisha uwazi, uwekaji wa tozo na riba, njia za ukusanyaji wa madeni, utunzaji wa taarifa binafsi za wateja na kulinda faragha zao.


Aidha, BOT imesema imechapisha na itaendelea kuhuisha orodha ya watoa huduma walioidhinishwa kutoa huduma za mikopo katika tovuti yake.

Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya ulinzi wa taarifa binafsi  Emmanuel Mkilia, mwezi Juni, 2024, alizionya taasisi na watu binafsi wanaofanya vitendo vya udhalilishaji kwa kuchukua taarifa za wateja wao akisisitiza kuwa ni kinyume cha sheria.

Katika Kikao cha Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Julai, 2024, aliyekuwa Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye alitoa Bungeni maelekezo kwa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Kitendo cha Uhalifu wa Mtandaoni kufuatilia na kuchunguza watu wanaotumia taarifa za waliowakopesha mtandaoni kudhalilisha.

#KAZIINAONGEA



Club News Editor

Comments

Popular posts from this blog

RC PWANI AONGOZA WAKAZI PWANI KUJIANDIKISHA KWENYE DAFTARI LA WAPIGA KURA

BARAZA LA MADIWANI KIBAHA MJINI LAMPONGEZA MKURUGENZI WAKE KWA KAZI NZURI ANAYOIFANYA SAMBAMBA NA KUONGEZA MAPATO.

RAIS SAMIA ATANGAZA KIBAHA MJINI KUWA MANISAPAA,MBUNGE KOKA AFURAHIA ASEMA KIBAHA ITANG'AA