SERIKALI KUTEKELEZA MIRADI MIKUBWA YA MAJI ZIWA VICTORIA, BILIONI 100 KUPELEKA UMEME KIGOMA VIJIJINI.



Na Gustaphu Haule, Tanzania 

SERIKALI ya awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan inaendelea kutekeleza miradi mikubwa miwili ya kutoa maji Ziwa Victoria ambayo ni Mradi wa Ziba-Nkinga wenye kuhudumia vijiji 9 na mradi wa Nkinga Simbo utakaohudumia vijiji 8 vilivyopo jimbo la Manonga Mkoani Tabora.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Maji Mhandisi Kundo Mathew wakati akijibu swali la Mbunge wa Jimbo la Manonga Seif Gulamali, aliyeuliza lini Serikali itatenga fedha za ujenzi wa miradi ya maji ya Ziwa Victoria katika kata ya Igoweko, Uswayu na Tambalale - Manonga.

Mhandisi Kundo amesema mipango ya Serikali ni kusambaza maji kupeleka katika Kata za Igoweko, Tambalale na Uswayu mara baada ya kukamilisha miradi hiyo.

Amesema  Serikali inaendelea na zoezi la uchimbaji visima na kujenga miundombinu rahisi ya kuchotea maji (Point source) kwa vijiji vya Igoweko, Mpogolo na Igondela vilivyoko katika kata ya Igoweko.


Katika hatua nyingine Serikali kupitia Wakala wa Nishati Vijijini(REA) imetumia  Sh.bilioni 100 kutekeleza miradi ya kupeleka umeme katika Vijiji mbalimbali vilivyopo Mkoani Kigoma.
 
Mkoa wa  Kigoma una jumla ya Vijiji 306 ambapo kati ya hivyo tayari  Vijiji  279 vimeunganishwa na nishati ya umeme na kwa sasa serikali inapeleka umeme kwenye vitongoji ambapo zaidi ya vitongoji 595 wakandarasi wanaendelea na utekelezaji wa mradi.
 
Aidha Katika vitongoji 1849 vya  Mkoa wa Kigoma, vitongoji Zaidi ya 1370 tayari vimeshapata umeme.

KAZIINAONGEA.


Club News Editor

Comments

Popular posts from this blog

BARAZA LA MADIWANI KIBAHA MJINI LAMPONGEZA MKURUGENZI WAKE KWA KAZI NZURI ANAYOIFANYA SAMBAMBA NA KUONGEZA MAPATO.

RAIS SAMIA ATANGAZA KIBAHA MJINI KUWA MANISAPAA,MBUNGE KOKA AFURAHIA ASEMA KIBAHA ITANG'AA

RC PWANI AFURAHISHWA NA UTENDAJI KAZI WA MKURUGENZI WA KIBAHA MJINI DKT.ROGERS SHEMWELEKWA