RAIS SAMIA KUKABIDHI HUNDI YA SH.BILIONI 6 KWA WATAFITI 16 WA MABADILIKO YA TABIA YA NCHI.
Na Gustaphu Haule,Tanzania
#KAZIINAONGEA
RAIS wa awamu ya sita, Dkt.Samia Suluhu Hassan, anatarajia kukabidhi hundi yenye thamani ya Shilingi Bilioni 6.3 kwa watafiti 16 wanaoshughulika na masuala ya mabadiliko ya tabia nchi.
Kwa kuzingatia umuhimu wa kuhimili mabadiliko ya Tabia ya nchi na kukuza uchumi shindani ambapo mwaka huu Serikali inataka kuonyesha jinsi bunifu za ndani zinavyoweza kuleta maendeleo endelevu.
Rais Dkt. Samia anatarajia kukabidhi hundi hiyo wakati wa uzinduzi wa mfuko wa mikopo wa kusaidia ubidhaishaji na ubiasharaishaji wa ubunifu na teknolojia zinazobuniwa na vijana wa Kitanzania.
Akielezea kuwepo kwa Kongamano hilo la tisa la Kitaifa la Sayansi, Teknolojia na Ubunifu Jijini Dodoma, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Adolf Nkenda amesema, kongamano hilo linatarajia kufanyika kuanzia Desenba 2 hadi 4, 2024.
Mfuko huo unaanza na kiasi cha Shilingi Bilioni 2.3 ambazo zitatumika kukopesha wabunifu kuendeleza kazi zao.
Katika kongamano hilo pia Rais anatarajia kuwatambua na kutoa tuzo kwa wanasayansi na wabunifu ambao matokeo ya kazi zao zimechangia kuleta maendeleo ya kiuchumi na kijamii ndani na nje ya nchi.

Comments
Post a Comment