RAIS SAMIA ALETA MAPINDUZI MAKUBWA ELIMU YA SEKONDARI



Na Gustaphu Haule, Tanzania 

#KAZIINAONGEA

KATIKA kipindi cha miaka mitatu ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan amefanikiwa kuleta mapinduzi makubwa kwenye  eneo la elimu ya Sekondari.

Dkt.Samia amefanikiwa kuboresha miundombinu iliyosaidia kuongeza idadi ya Wanafunzi wa kidato cha kwanza hadi cha nne kutoka 2,256,489 mwaka 2021 hadi wanafunzi 2,881,335 Februari 2024 sawa na ongezeko la wanafunzi 624,846.

 Aidha wanafunzi wa kidato cha Tano na Sita wameongezeka kutoka 123,456 mwaka 2021 hadi kufikia Wanafunzi 159,816 mwezi Februari, 2023 sawa na ongezeko la wanafunzi 36,360.

Ongezeko la Sekondari .

Shule za Sekondari, zimeongezeka kutoka Shule 4,002 mwaka, 2021 hadi kufikia Shule 4,510 Februari, 2024 sawa na ongezeko la shule 508.



Mradi wa SEQUIP
Katika mradi wa kuboresha elimu ya Sekondari (SEQUIP) jumla ya Shilingi Bilioni 381.7 zimetumika katika ujenzi wa miundombinu ya elimu kwa shule za sekondari kupitia Mradi wa SEQUIP na kujenga miundombinu ifuatayo.


Ujenzi wa shule  460 za kata,ujenzi wa shule 26 za bweni za Kitaifa,upanuzi wa shule kongwe 18 za kidato cha tano na sita,ukamilishaji wa maboma ya madarasa, matundu ya vyoo 1,650 na maabara 132,ujenzi wa nyumba za Walimu zenye uwezo wa kuchukua familia 424 na ukarabati wa shule chakavu. 
 

Katika eneo la mradi wa Boost.

Kwenye eneo la mradi wa kuboresha elimu ya msingi (BOOST) Serikali kupitia mradi huo imetuma fedha katika Mamlaka za Serikali za Mitaa kiasi cha Shilingi bilioni 230 kwa ajili ya ujenzi wa Shule mpya za awali na Msingi 302.



Mradi huo umefanikiwa kujenga vyumba vya madarasa 3,880, matundu ya vyoo 11,297, nyumba za walimu 41, mabweni 2 na ukarabati wa Shule za Msingi 4. 

Baadhi ya madarasa yanayotokana na mradi wa BOOST

Ujenzi wa madarasa kupitia tozo,Serikali kuu na Uviko -19

Mwaka 2021 watoto waliomaliza darasa la saba walikuwa ni mara mbili ya wanaomaliza kidato cha nne na kukawa na uhaba mkubwa wa vyumba vya madarasa, Rais Samia akatoa  fedha kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa 12,000 .

Ujenzi wa madarasa hayo yakawezesha kuchukua wanafunzi wote waliofaulu kuingia kidato cha kwanza kwa awamu moja jambo ambalo limekuwa na msaada mkubwa katika jamii.

Mbali na hilo lakini pia  Rais Samia akaiona adha ya wanafunzi wa msingi waliokua wanasoma katika vituo shikizi ambapo akatoa fedha za kujenga vyumba vya madarasa 3,000 katika vituo hivyo na kwa sasa vina mazingira bora ya kujifunzia na kufundishia.

Mradi wa GPE Lanes II.

Kupitia mfumo wa ujenzi wa miundombinu kazi mbalimbali zimefanyika kwa kupitia fedha hizo  ikiwemo uenzi wa madarasa 300 ya elimu ya Awali ya mfano, ujenzi wa hosteli 20 za Wanafunzi wenye mahitaji maalumu, ujenzi wa madarasa 432, matundu ya vyoo 932, nyumba za Walimu 11, mabweni 8 na Shule mpya 10.


Kuhusu ununuzi wa magari.

Serikali ya Awamu ya Sita kupitia miradi mbalimbali imefanikisha kununua magari 445 kwa ajili ya maafisa elimu Mkoa, Wakuu wa divisheni za Msingi na Sekondari na magari kwa matumizi ngazi ya Wizara kwa lengo likiwa  ni kuimarisha shughuli za ufuatiliaji na tathmini ya utekelezaji wa Elimu hapa nchini.



Hatahivyo,taarifa hii ni kwa mujibu wa muhtasari wa mafanikio ya miaka mitatu ya Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Samia tangu aingie madarakani uliotolewa na Tamisemi.

Club News Editor

Comments

Popular posts from this blog

BARAZA LA MADIWANI KIBAHA MJINI LAMPONGEZA MKURUGENZI WAKE KWA KAZI NZURI ANAYOIFANYA SAMBAMBA NA KUONGEZA MAPATO.

RAIS SAMIA ATANGAZA KIBAHA MJINI KUWA MANISAPAA,MBUNGE KOKA AFURAHIA ASEMA KIBAHA ITANG'AA

RC PWANI AFURAHISHWA NA UTENDAJI KAZI WA MKURUGENZI WA KIBAHA MJINI DKT.ROGERS SHEMWELEKWA