RAIS SAMIA AFANYA MAPINDUZI MAKUBWA YA KIMAENDELEO SEKTA YA AFYA , HALMASHURI 127 ZAPATA HOSPITALI MPYA.


Na Gustaphu Haule, Tanzania 

KATIKA  kipindi kifupi cha uongozi wa  Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, amefanikiwa kufanya  mapinduzi makubwa kwenye sekta ya afya nchini kwa kujenga na kufanya uendelezaji wa hospitali mpya za Halmashauri 127.

Mapinduzi hayo yametokana na uwekezaji mkubwa uliofanywa kwenye uboreshaji wa  miundombinu ya kutolea huduma za afya ya msingi, vifaa tiba na vitendanishi, watumishi pamoja na upatikanaji wa dawa katika vituo vya kutolea huduma za afya nchini.



Serikali ya awamu ya Sita imeanzisha ujenzi na uendelezaji wa hospitali mpya za Halmashauri 127 ambazo kati ya hizo Hospitali 25 zimeanza kujengwa katika kipindi cha awamu ya sita. 

Ukarabati wa hospitali Kongwe 50 za Halmashauri,ujenzi wa vituo vya afya 367, ikijumuisha vituo vya tozo 234 na ukamilishaji wa maboma ya Zahanati 980 na ameanzisha ujenzi wa majengo 83 ya kutolea huduma za dharura (EMD).



Ujenzi wa majengo 28 ya huduma kwa wagonjwa mahututi (ICU), ujenzi wa Kituo cha kutibu magonjwa ya milipuko na ujenzi wa mitambo 21 ya kuzalisha hewa Tiba ya oksijeni kwa ajili ya wagonjwa mahututi na Wagonjwa wa dharura.

Pia amejenga nyumba za Watumishi 270 ( 3 in 1), ununuzi wa Vifaa Tiba kwenye Zahanati, Vituo vya Afya na Hospitali na kuajiri watumishi wa kada mbalimbali za Afya 17,137

Mapinduzi haya yanadhihirishwa na namna alivyosogeza baadhi ya huduma muhimu kwenye maeneo mbalimbali, hasa huduma za EMD na ICU.

Ikumbukwe kuwa tangu nchi hii inapata uhuru vituo vya kutolea huduma za afya yaani (Zahanati, vituo vya afya  pamoja na hospitali za Wilaya)  havijawahi kuwa na majengo ya dharura (EMD), majengo ya wagonjwa mahututi (ICU) pamoja Mitambo ya kuzalisha hewa Tiba ya Oksijeni.


Katika kipindi cha miaka mitatu Rais Dkt. Samia amelifanikisha hilo na huduma hiyo leo imekua ni kitu cha msingi ambacho kinapatikana katika vituo 132 hapa nchini.

Kwa mujibu wa Takwimu za Tamisemi asilimia 75% ya Watanzania wote wanatibiwa kwenye vituo vya kutolea huduma za afya nchini lakini pia asilimia 80 ya Wajawazito wote wanajifungua kwenye vituo vya kutolea huduma za Afya.

Taarifa hii ni kwa mujibu wa muhtasari wa mafanikio ya miaka mitatu ya Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Samia tangu aingie madarakani uliotolewa na Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI).

#KAZIINAONGEA
Club News Editor - Charles Kusaga

Comments

Popular posts from this blog

RC PWANI AONGOZA WAKAZI PWANI KUJIANDIKISHA KWENYE DAFTARI LA WAPIGA KURA

BARAZA LA MADIWANI KIBAHA MJINI LAMPONGEZA MKURUGENZI WAKE KWA KAZI NZURI ANAYOIFANYA SAMBAMBA NA KUONGEZA MAPATO.

RAIS SAMIA ATANGAZA KIBAHA MJINI KUWA MANISAPAA,MBUNGE KOKA AFURAHIA ASEMA KIBAHA ITANG'AA