RAIS SAMIA AAGIZA KUFANYIKA UKAGUZI MAGHOROFA KARIAKOO



Na Mwandishi wetu

*●Rais Dkt.Samia aagiza ukaguzi maghorofa yote* 

 WAKATI Serikali ikiendelea na zoezi la uokoaji katika ghorofa lililoanguka Kariakoo, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amezitaka mamlaka zinazohusika kuchukua hatua stahiki ikiwemo ya kuyafanyia ukaguzi majengo ya ghorofa yaliyojengwa na yanayoendelea kujengwa ili kubaini uimara wake.


 Dkt. Samia ametoa maagizo hayo katika taarifa yake kwa umma kuhusiana na ajali ya kuporomoka kwa jengo la ghorofa maeneo ya Kariakoo jijini Dar es Salam hivi karibuni. 



 Alieleza kuwa hatuna hiyo itasaidia kubaini ubora wa majengo hayo na kuepusha madhara kwa watu na mali zao. 

 Aidha amelitaka Jeshi la polisi kumuhoji mmiliki wa jengo hilo ili kusaidia uchunguzi na kupata ukweli juu ya sababu za kuporomoka kwa jengo hilo. 

 Aidha Dkt. Samia amempongeza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na vyombo vya ulinzi, wadau mbalimbali na wananchi kwa kushiriki katika uokoaji na kuahidi serikali kugharamia matibabu pamoja na mazishi ya watu waliopoteza maisha. 





 Pia Dkt. Samia ametoa pole kwa ndugu, jamaa na marafiki wa watu waliofariki katika mkasa huo na kuwatakia ahueni ya haraka manusura wa tukio hilo ambao hadi Jumapili Novemba 17 jumla ya watu 13 walithibitishwa kufariki dunia. 

 #KAZIINAONGEA 

Club News Editor - Charles Kusaga






Comments

Popular posts from this blog

BARAZA LA MADIWANI KIBAHA MJINI LAMPONGEZA MKURUGENZI WAKE KWA KAZI NZURI ANAYOIFANYA SAMBAMBA NA KUONGEZA MAPATO.

RAIS SAMIA ATANGAZA KIBAHA MJINI KUWA MANISAPAA,MBUNGE KOKA AFURAHIA ASEMA KIBAHA ITANG'AA

RC PWANI AFURAHISHWA NA UTENDAJI KAZI WA MKURUGENZI WA KIBAHA MJINI DKT.ROGERS SHEMWELEKWA