Skip to main content

MTAMBO WA KISASA WA UCHAKATAJI DHAHABU WAZINDULIWA SONGWE


Na Gustaphu Haule, Tanzania 

#KAZIINAONGEA

MAZINGIRA mazuri na wezeshi ya uwekezaji yaliyowekwa na Serikali ya awamu ya Sita, inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan yamesaidia Tanzania kuendelea kuongeza mitambo ya uchakataji na uchenjuaji wa dhahabu.

Novemba 17,2024 Mkuu wa Wilaya ya Songwe, Solomon Itunda amezindua kiwanda na mtambo wa kisasa wa uchakataji na uchenjuaji wa dhahabu unaotumia teknolojia ya Carbon-In-Pulp (CIP) wenye thamani ya zaidi ya Shilingi 10 bilioni 



Mtambo huo unamilikiwa na mwekezaji mzawa, Fredrick Ashery Meshack kupitia Kampuni ya Green Pacific Invistement Limited katika Kata ya Mbangala Wilayani Songwe. 

Uzinduzi huo umefanyika katika eneo la mradi lililopo Kata ya Mbangala Wilaya ya Songwe ambapo Itunda ametumia nafasi hiyo kumpongeza mwekezaji huyo mzawa kwa kuthubutu na kufanya uwekezaji mkubwa katika wilaya hiyo.

Itunda amesema kuwa, mwekezaji huyo amekuwa kijana mwenye mipango anayeziishi ndoto zake huku akitoa wito kwa vijana kujifunza kwake ili kupata wawekezaji wengine katika sekta ya madini wilayani humo.

Mkuu huyo wa Wilaya huyo  amesema kuwa uwekezaji huo unatokana na mazingira mazuri yaliyowekwa na Rais Dkt. Samia kwa wawekezaji wa ndani na nje ya nchi.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, mwekezaji huyo ameishukuru  Serikali na Benki ya NMB kwa kuwezesha mkopo wa zaidi ya Sh bilioni 10 fedha ambazo zimetumika kujenga mtambo huo.


Ametoa wito kwa wachimbaji na vijana kutokata tamaa huku akisema  anaamini kuwa inawezekana kufikia malengo kama mtu atayasimamia huku akiwashauri vijana kuacha kuogopa.

Aidha, Itunda amewataka wachimbaji kujenga mahusianbo mazuri na uaminifu kwa taasisi za fedha ili kuweza kutengeneza mazingira ya kukopesheka na kufanya uwekezaji.

Kuanzishwa kwa mtambo  huo kutasaidia kuchangia mapato katika mfuko mkuu wa Serikali ya zaidi ya Shilingi bilioni 2 kwa mwaka na kuzalisha ajira zaidi ya 200 kwa wananchi wa Songwe na Tanzania kwa ujumla.

#KAZIINAONGEA

Club News Editor

Comments

Popular posts from this blog

BARAZA LA MADIWANI KIBAHA MJINI LAMPONGEZA MKURUGENZI WAKE KWA KAZI NZURI ANAYOIFANYA SAMBAMBA NA KUONGEZA MAPATO.

RC PWANI AFURAHISHWA NA UTENDAJI KAZI WA MKURUGENZI WA KIBAHA MJINI DKT.ROGERS SHEMWELEKWA

TANROADS YATOA UFAFANUZI KUTOZWA FAINI GARI LA SIMBA LOGISTICS KITUO CHA MIZANI YA VIGWAZA MKOA WA PWANI