GHARAMA YA NISHATI KUSHUKA,TANZANIA YAVUTIA WAWEKEZAJI WA AFRIKA


Na Gustaphu Haule,Tanzania
 
#KAZIINAONGEA

KATIKA kuhakikisha gharama za nishati zinashuka nchini, Serikali ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imewaalika wawekezaji kutoka nje kuja nchini kuwekeza katika sekta ya nishati kwa kuwa Tanzania zipo fursa nyingi.

Mwaliko huo umetolewa Novemba 5, 2024, katika mkutano wa Wiki ya Nishati Afrika iliyofanyika nchini Afrika Kusini.


Ofisi ya Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati anayeshughulikia masuala ya mafuta na gesi ambayo imebainisha kuwa fursa zilizopo katika sekta hiyo ni vitalu vya utafutaji wa mafuta na gesi asilia, miundombinu ya mafuta na gesi, miradi ya nishati jadifu na viwanda vya petrokemikali.
 
Kwa upande wa vitalu vya utafutaji wa mafuta na gesi asilia tayari Wizara ya Nishati imekamilisha maandalizi muhimu kuelekea tukio la uzinduzi wa duru ya tano ya kunadi vitalu vya mafuta na gesi asilia vilivyo wazi ambao utaanza rasmi Machi, 2025 wakati wa mkutano na maonesho ya Petroli ya Afrika Mashariki utakaofanyika jijini Dar es Salaam.
 
Tanzania itanadi Jumla  ya vitalu 26 vya utafutaji wa mafuta na gesi asilia nchini. Kati ya vitalu hivyo, vitalu 23 vipo eneo la baharini na vitatu vipo eneo la Ziwa Tanganyika.
 

Pamoja na vitalu hivyo, ipo fursa kwa wawekezaji kushirikiana na Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) kuendeleza vitalu vya Eyasi-Wembere, Mnazi Bay Kaskazini na Songo Songo Magharibi; vitalu ambavyo TPDC imeendelea kuvifanyia utafiti wa mafuta na gesi asilia.
 
Aidha vitalu vyote vitakavyowekwa sokoni ni vile vinavyoendeshwa na TPDC kwa lengo la wawekezaji kuona na kushiriki mnada huo kikamilifu.
 
Maeneo mengine ya uwekezaji katika sekta ya gesi asilia ni uwekezaji katika ujenzi wa vituo vya kujaza gesi asilia kwenye magari na viwanda vya petrokemikali kwa kutumia gesi asilia.
 
Serikali ya Rais Samia imefanya kazi kubwa ya kuboresha mazingira ya uwekezaji nchini na kutekeleza miradi ya kimkakati kama vile Bwawa la kuzalisha Umeme la Mwalimu Julius Nyerere (JNHPP), hivyo Tanzania ni sehemu sahihi kwa uwekezaji.


Club News Editor

Comments

Popular posts from this blog

BARAZA LA MADIWANI KIBAHA MJINI LAMPONGEZA MKURUGENZI WAKE KWA KAZI NZURI ANAYOIFANYA SAMBAMBA NA KUONGEZA MAPATO.

RAIS SAMIA ATANGAZA KIBAHA MJINI KUWA MANISAPAA,MBUNGE KOKA AFURAHIA ASEMA KIBAHA ITANG'AA

RC PWANI AFURAHISHWA NA UTENDAJI KAZI WA MKURUGENZI WA KIBAHA MJINI DKT.ROGERS SHEMWELEKWA