FILAMU YA ROYAL TOUR YAFANIKIWA KUVUTIA WAWEKEZAJI NCHINI, HIFADHI ZA TAIFA ZAVUNJA REKONDI
Na Gustaphu Haule,Tanzania
#KAZIINAONGEA
KUWEPO kwa filamu ya Royal Tour iliyotengenezwa kutokana na maono ya Rais wa awamu ya sita, Dkt.Samia Suluhu Hassan, imesaidia kuongeza mwamko wa wawekezaji kuja kuwekeza kwenye Sekta ya Madini nchini.
Filamu hii iliyoonekana kuvutia katika Sekta ya Utalii nchini imewavutia wageni kuja kuwekeza katika Madini, na Taifa linajivunia uwekezaji katika sekta hiyo kwa kuwa Tanzania tuna madini ya kutosha.
Kufuatia filamu ya Royal Tour watu bilioni 1.2 wamehusika moja kwa moja kuona, kutazama, kuangalia na kuifuatilia Tanzania kutokana na filamu hiyo kutangazwa na Rais Dkt. Samia.
Filamu hiyo imekuwa na mafanikio makubwa na kusababisha Hifadhi za Taifa kuvunja rekodi kwa kupata jumla ya watalii 1,412,719 kwa kipindi cha miezi tisa idadi ambayo haijawai kufikiwa.
Aidha, kumekuwa na ongezeko la mapato ya utalii maradufu ambapo mapato ya jumla ya sekta yameongezeka kutoka Dola za Kimarekani bilioni 1.310.34 sawa na Tsh. Trilioni 3.01 mwaka 2021 hadi Dola za Marekani bilioni 2.527.77 sawa na Tsh .bilioni 5.82).
Ni ukweli usiopingika kuwa, Tanzania imejaliwa kuwa na madini aina nyingi na kuwepo kwa madini hayo kumesaidia ongezeko la wazalishaji wadogo, wa kati na wakubwa, hivyo kabla ya mwekezaji kufanya shughuli za uchimbaji ni lazima afuate masharti ya uwekezaji.
Moja ya masharti hayo ni kwa kuandaa taarifa ya athari za mazingira wakati wa uchimbaji madini na namna ya kurejesha katika hali yake ya asili baada ya uchimbaji ambapo Madini kama Uranium tathmini yake inafanyika kwa mapana zaidi.
Katika kusimamia Uwekezaji na shughuli za uchimbaji wa madini, Wizara ya Madini ina vitengo vyote vinavyosimamia masuala ya afya, usalama, na utunzaji mazingira kikiwemo cha ukaguzi wa migodi.
Serikali imefanya uwekezaji mkubwa katika Sekta ya Madini kwa kununua mitambo mikubwa mitano ambayo ilishawasili nchini na kumi ipo njiani inakuja.
Rais Dkt. Samia ameagiza kuletwa kwa mitambo hiyo itakayowarahisishia wachimbaji wadogo kupata taarifa za uchimbaji na kuwaepusha na hasara.
Rais ameagiza mitambo hii ikifika igawanywe kote ambapo miongoni mwa mitambo hiyo itengwe miwili kwa ajili ya vijana na mmoja kwa ajili ya wanawake.
Mpango wa Serikali ni kuhakikisha kuwa sekta hii inachangia asilimia 10 au zaidi katika Pato la Taifa ifikapo 2025 na ukuaji wa Sekta ya Madini umeongezeka kutoka asilimia 9.4 Mwaka 2021 hadi kufikia asilimia 11.3 Mwaka 2023.
Kutokana na kuendelea kuimarika kwa Sekta, mchango wa Sekta ya Madini katika Pato la Taifa utaongezeka na kufikia asilimia 10 au zaidi ifikapo Mwaka 2025 kama ilivyoelezwa katika Dira ya Maendeleo ya Taifa 2025.
Serikali kupitia Tume ya Madini inarudisha minada ya ndani ya madini ya vito itakayofanyika katika maeneo ya uzalishaji hususani Mirerani, Mahenge, Tunduru, Dar es Salaam, Arusha na Tanga ambapo Kimataifa itafanyika Mji wa Bangkok na Jaipur nchini India.
Uendeshaji wa minada hiyo ni fursa muhimu ya kutangaza madini ya vito yanayozalishwa hususan kwenye Masoko ya Kimataifa ambayo ni njia mojawapo ya kuwafikisha Watanzania katika masoko ya uhakika na upatikanaji wa bei nzuri na stahiki.
#KAZIINAONGEA



Comments
Post a Comment