WAZIRI BASHUNGWA ARIDHISHWA NA USIMAMIZI WA MIRADI BAGAMOYO, AMTAJA RAIS SAMIA KUWA KINARA WA MAENDELEO NCHINI.
Na Gustaphu Haule, Bagamoyo
Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo Shauri Salenda (Kushoto)akimueleza jambo Waziri wa Ujenzi Innocent Bashungwa (katikati) alipokuwa akikagua Soko la Samaki la Bagamoyo jana na Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakar Kunenge.
WAZIRI wa Ujenzi Innocent Bashungwa amefanya ziara Wilayani Bagamoyo kwa ajili ya kukagua na kuzindua miradi mbalimbali ya maendeleo iliyotekelezwa kwa kipindi cha miaka mitatu ya Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan.
Bashungwa, amefanya ziara hiyo Wilayani humo ikiwa ni siku yake ya pili tangu alipoanza ziara yake Oktoba 8 katika Halmashauri ya Kibaha Mjini na Halmashauri ya Kibaha Vijijini.
Waziri Bashungwa aliambatana na mwenyeji wake Mkuu wa Mkoa wa Pwani amefika katika Soko la samaki lililopo Wilayani Bagamoyo kwa ajili ya kuzungumza na wavuvi wa Soko hilo na kisha kujua changamoto mbalimbali zinazowakabili.
Waziri wa Ujenzi Innocent Bashungwa katika Soko la Samaki Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo Mkoani Pwani katika ziara yake aliyoifanya Oktoba 9 katika Halmashauri hiyo.
Mbali na kufika sokoni hapo lakini pia Bashungwa amezindua Shule mpya ya Sekondari ya Nianjema pamoja na kutembelea kipande cha barabara ya lami ya Nianjema.
Akizungumza katika ziara hiyo Bashungwa amesema kuwa katika kipindi kifupi cha uongozi wa Rais Samia Serikali imefanya kazi kubwa ya kuwaletea Wananchi maendeleo na mafanikio hayo yanatokana na Rais kukubali kutoa fedha kwa ajili ya utekelezaji wa miradi hiyo.
Bashungwa, amesema kuwa kwa Mkoa wa Pwani pekee mpaka sasa Serikali imetoa kiasi cha Sh Trilioni 1.3 lakini licha ya fedha hizo kutolewa lakini bado fedha nyingine zinakuja.
Waziri wa Ujenzi Innocent Bashungwa (Kulia) pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakar Kunenge (kushoto) wakishiriki ujenzi wa Shule mpya ya Sekondari Nianjema iliyopo Wilayani Bagamoyo,Bashungwa alifanya ziara Wilayani humo Oktoba 9 Kwa ajili ya kukagua miradi mbalimbali.
"Nafanya ziara hii maalum kwa ajili ya kukagua miradi yote ya maendeleo ambayo imepata fedha kutoka kwa Rais Samia na ziara pia ni maelekezo yake kwakuwa anataka kujua fedha alizotoa kama zimefanyakazi iliyokusudiwa", amesema Bashungwa
Bashungwa, amesema kwa Wilaya ya Bagamoyo ameona kazi kubwa imefanyika kiasi ambacho kinampa nguvu Rais kuendelea kutoa fedha kwa ajili ya kutekeleza miradi mingine ya maendeleo.
Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo Shauri Salenda (Kushoto)akimueleza jambo Waziri wa Ujenzi Innocent Bashungwa (katikati) alipokuwa akikagua Soko la Samaki la Bagamoyo jana na Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakar Kunenge.Aidha, amewaomba Wananchi waliopo Wilayani Bagamoyo kuendelea kumpa ushirikiano Rais Samia ili kuhakikisha anaongeza nguvu ya kuleta fedha nyingi zaidi kwa ajili ya kuhakikisha changamoto zilizopo zinamalizwa.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakar Kunenge amemshukuru Rais Samia kwa namna alivyojitoa katika kutoa kipaumbele cha kutoa fedha nyingi kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo.
Kunenge,amesema kuwa kwasasa Mkoa wa Pwani umefungua na umekuwa na fursa nyingi za kiuchumi ambapo amewataka wawekezaji kujitokeza zaidi katika kufanya uwekezaji kwakuwa tayari kuna mazingira mazuri na wezeshi yaliyotokana na juhudi za Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo Shauri Salenda,amesema anaishukuru Serikali kwa jitahada kubwa inazofanya kwani katika kipindi kifupi Halmashauri yake imefanikiwa kujenga miradi mingi na mikubwa yenye kurahisisha huduma kwa Wananchi.
Waziri wa Ujenzi Innocent Bashungwa wa tatu kutoka kulia akiambatana na viongozi mbalimbali kwa ajili ya kukagua miradi ya barabara Wilayani Bagamoyo ambapo Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakar Kunenge na anayefuatia ni Meneja Tanroads Mkoa wa Pwani Baraka Mwambage .
Hatahivyo, Salenda amemshukuru Waziri Bashungwa kwa kufanya ziara hiyo katika Halmashauri yake huku akiahidi kuendelea kushirikiana na watumishi wake kusimamia miradi kikamilifu.




Comments
Post a Comment