RAIS SAMIA ATOA MIKOPO ISIYO NA MASHARTI NGAZI YA KATA NCHINI



Na. Gustaphu Haule, Tanzania 

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ameanzisha mpango maalum wa kutoa mikopo isiyo na masharti kwa wananchi wasiojiweza kuanzia ngazi ya Kata.

Rais Samia ametoa fursa hiyo akiwalenga zaidi  vijana walio na umri wa kuanzia miaka 18 hadi 45 kwa jinsia zote, wanawake  na walemavu.  



Wanufaika wa mkopo huo watalazimika kulipa riba ndogo iliyogawanywa  katika makundi matatu, ambapo kundi la vijana litalipa asilimia nne, wanawake asilimia nne na kundi la walemavu litalipa  asilimia mbili.


Mpango huo ni endelevu uliolenga kuwasaidia wananchi wote wenye kipato cha chini ili kujikwamua kiuchumi.

Katika kuhakikisha hakuna vikwazo hatua zote za kisheria kwa wananchi kwa ajili ya kuchukua mkopo huo  zimerahisishwa na  hakuna kulipia gharama zozote za awali.

Mkopo huu umewalenga Watanzania wa maeneo yote mijini na vijijini.

Club News Editor - Charles Kusaga





Comments

  1. Umetudanganya hizo asilimia za riba siyo kweli.
    Ukweli ni kwamba miko hii inatokana na 10% ya Mapatato ya ndani ya Halmashauri.
    Mgawanyo wake ndiyo huo 4% Wanawake
    4%Vijana na 2% Walemavu.

    ReplyDelete

Post a Comment

Popular posts from this blog

RC PWANI AONGOZA WAKAZI PWANI KUJIANDIKISHA KWENYE DAFTARI LA WAPIGA KURA

BARAZA LA MADIWANI KIBAHA MJINI LAMPONGEZA MKURUGENZI WAKE KWA KAZI NZURI ANAYOIFANYA SAMBAMBA NA KUONGEZA MAPATO.

RAIS SAMIA ATANGAZA KIBAHA MJINI KUWA MANISAPAA,MBUNGE KOKA AFURAHIA ASEMA KIBAHA ITANG'AA