RC KUNENGE: WAKUU WA WILAYA FANYENI MAAMUZI SAHIHI


Na Gustaphu Haule, Pwani

MKUU wa mkoa wa Pwani Abubakari Kunenge, amesema Wakuu wa wilaya  wanatakiwa kufanyakazi kwa bidii  sambamba na kufanya maamuzi sahihi ambayo yatachochea ukuaji wa maendeleo katika wilaya  zao.


Kunenge  ametoa maagizo hayo Septemba 5, mwaka huu Mjini Kibaha wakati wa hafla fupi ya kumuapisha mkuu mpya wa Wilaya ya Rufiji Luteni Kanali Fredrick Komba ambaye ameteuliwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan hivi karibuni.



Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakar Kunenge akimuapisha na kumkabidhi vitendeakazi Mkuu wa Wilaya ya Rufiji Luteni Kanali Fredrick Komba katika hafla iliyofanyika Septemba 5,2024 katika jengo la ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani lililopo Mjini Kibaha.

Amesema kuwa, kwa nafasi walizonazo wanapaswa kutambua kuwa yapo mambo ambavyo wanaruhusiwa kufanya na yale ambayo hawaruhusiwi kufanya lakini wapo wengine ambao wanadhani ukiwa kiongozi basi ni kila kitu jambo ambalo sio sahihi 

Amesema, kinachotakiwa ni kuhakikisha Mkuu wa Wilaya anafanya au kiongozi anafanya mambo ambayo yanachangia maendeleo na wakitaka kufanikiwa ni vizuri wakatoa ushirikiano kwa watumishi wao .

"Nataka Wakuu wote wa Wilaya kufanya mambo kulingana na uwezo wenu na hata kufanya maamuzi yenye kuleta matokeo chanya ya kimaendeleo na mkitaka kufanikiwa zaidi jengeni ushirikiano na watumishi wenu na hata Wananchi," amesema Kunenge 

Baadhi ya Wakuu wa Wilaya wa Mkoa wa Pwani na viongozi wengine wakishuhudia hafla ya kuapishwa kwa Mkuu wa Wilaya ya Rufiji Luteni Kanali Fredrick Komba iliyofanyika Septemba 5, Mjini Kibaha.



Kunenge, ameahidi kuendelea kutoa ushirikiano kwa Mkuu wa Wilaya ya Rufiji Luteni Kanali Fredrick Komba huku akisema Mkoa wa Pwani ni Mkoa wa viwanda ,uwekezaji na hata kilimo hivyo lazima jitihada zifanyike ili kufikia malengo.

Aidha, Kunenge amewataka viongozi hao  kufanya kazi kwa uadilifu ikiwa pamoja na kuondoa urasimu kwa wawekezaji na hata shughuli nyingine za maendeleo na kuhakikisha wanasimamia ilani ya CCM kwa vitendo.

Kwa upande wake mkuu wa Wilaya ya Rufiji Luteni Kanali Fredrick Komba,amemshukuru Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kumteua kuwa Mkuu wa Wilaya ya Rufiji na atakwenda kufanyakazi kwa bidii ili kufikia kutimiza malengo ya Rais .

Luteni Kanali Fredrick Komba akila kiapo kutumikia nafasi ya Ukuu wa Wilaya ya Rufiji baada ya kuteuliwa juzi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan,hafla ya kuapishwa kwake imefanyika Septemba 5,2024 Mjini Kibaha.



"Natambua dhamana niliyopewa ni kubwa kwahiyo nitakwenda kutekeleza yale ambayo Rais Samia alikusudia yafanyike Wilayani Rufiji lakini kikubwa ni ushirikiano baina ya watumishi na wananchi  waliopo ndani ya Wilaya yangu,"amesema Komba

Awali Katibu Tawala wa Mkoa wa Pwani Rashid Mchata ,amesema kuwa amewataka wakuu wa Wilaya kufanyakazi kwa kuzingatia Sheria, utaratibu na kikubwa zaidi ni kuwa na busara katika kazi.

Hatahivyo,Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Nickson John akizungumza kwa niaba ya mwenyekiti wa Wakuu wa Wilaya wa Mkoa wa Pwani Hadija Nasri amesema wao wanafanyakazi kwa timu na wanapima kazi zao kwa mifano ya matokeo ambapo huku akiahidi kutoa ushirikiano kwa Mkuu  wa Wilaya ya Rufiji.

Charles Kusaga - Editor

Comments

Popular posts from this blog

BARAZA LA MADIWANI KIBAHA MJINI LAMPONGEZA MKURUGENZI WAKE KWA KAZI NZURI ANAYOIFANYA SAMBAMBA NA KUONGEZA MAPATO.

RAIS SAMIA ATANGAZA KIBAHA MJINI KUWA MANISAPAA,MBUNGE KOKA AFURAHIA ASEMA KIBAHA ITANG'AA

RC PWANI AFURAHISHWA NA UTENDAJI KAZI WA MKURUGENZI WA KIBAHA MJINI DKT.ROGERS SHEMWELEKWA