KIKWETE AFANYA MAZUNGUMZO NA SHIRIKA LA KIMATAIFA LA KAZI (ILO)
Na. Julieth Ngarabali, PWANI
Ridhiwani Kikwete, Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, amekutana na kufanya mazungumzo na Mwakilishi mkazi wa Kanda ya Afrika Mashariki wa Shirika la Kazi (ILO) Bi. Caroline Mugalla na mratibu wa Mipango ya Kitaifa wa shirika hilo Bw. Edmund Moshy mchana leo , ofisini kwake Dodoma.
Katika mkutano huo , wamekubaliana kuendeleza mashirikiano baina yao na kuwahakikishia utayari wao kuendelea kufanyia kazi maamuzi makubwa yaliyoingiwa na Nchi yetu katika kusimamia maslahi mapana ya Wafanyakazi katika kada zote. #KaziInaendelea



Comments
Post a Comment