WANAOJIFUNGUA WATOTO NJITI WALIA NA SHERIA YA AJIRA NA MAHUSIANO KAZINI,


  • Watoto Njiti ni wale wanaozaliwa kabla ya miezi tisa ya ujauzito.
  •  Soma chanzo cha kuzaliwa , changamoto zao.

Julieth Ngarabali, Pwani.

 Wafanya kazi  wanawake  waliojifungua watoto kabla ya muda  wake maarufu watoto  njiti  wamesema siku 84 zilizowekwa kisheria kama likizo ya uzazi hazitoshelezi  kulea  watoto njiti  na kwamba kuna umuhimu wa Serikali kuangalia upya  uwezekano wa kuboresha sheria ya ajira na mahusiano kazini  sura ya 366 na marekebisho yake ya mwaka 2019 .

Katika sheria hiyo kifungu kidogo cha 33 kifungu kidogo cha 6 (a ) kinasema mtumishi mwanamke aliyejifungua mtoto mmoja atapata likizo ya siku 84  huku kifungu cha 33 kifungu kidogo cha 6 ( b ) inaeleza kuwa mtumishi mwanamke aliyejifungua watoto zaidi ya mmoja atapata likizo ya siku 100 ambapo sheria hiyo imeishia hapo haijasema kama atajifungua watoto njiti atapata muda wa ziada na hivyo shida imeanzia hapo 

Mmoja wa wanawake waliowahi kujifugua mtoto njiti ambaye pia ni mtumishi katika  Hospitali  ya rufaa ya mkoa wa Pwani yaTumbi  Felister Assenga  amesema  malezi ya  watoto wanaozaliwa kabla ya wakati  yanahitaji nafasi na muda wa kutosha wa kuwa karibu nao zaidi.

Mmoja wa waliowahi kujifungua mtoto njiti ambaye pia ni Afisa  muuguzi Hospitali ya Rufaa Tumbi Felister  Assenga  

"kiukweli kwa mwanamke liyejifungua mtoto njiti na huku ni mfanyakazi hizi siku 84 tunazopata  ni chache mno ikumbukwe kwamba kumuacha kichanga aliyezaliwa kabla ya miezi tisa na kwenda kazini  ni sawa na ukatili tu maana huyu mtoto anakuwa hajatengamaa vizuri  anahitaji ukaribu muda mwingi wa mama” anasema

Ni vema Serikali na wadau wa Afya wakaliona hili ili kuweza kuifanyiia maboresho tena sheria  hii ya ajira na mahusiano kazini na kwamba kama muhanga nashauri mtumishi anayejifungua mtoto njiti basi sheria iruhusu mzazi huyo akae miezi inayotimiza kipindi cha kujifungua mfano mjamzito amejifungua ndani ya miezi saba basi likizo yake ya siku 84 ijumlishwe na miezi miwili.

Chanzo cha kuzaliwa watoto njiti .

Kwa mujibu wa shirika la Afya Duniani (WHO) maradhi katika njia ya mkojo (UTI ) wanawake wenye historia ya kupatwa na uchungu mapemawapo katika hatari ya kujifungua njiti ukilinganisha na wasio na historia hiyo, kuwa na mimba yenye zaidi ya mtoto mmoja ,wanawake wenye matatizo katika maumbile ya mfumo wa uzazi nao wapo katika hatari zaidi, maradhi yanayosabishwa na ngono zembe ikiwemo Ukimwi,kisonono ,kaswende na trikomonasi.

Ingine ni shinikizo la damu ,kutokwa na damu katika sehemu za uzazi ,mama kuwa na uzito mdogo  au mkubwa kupitiliza wakati wa ujauzito,wanawake walio na umri unaozidi miaka 35 wapo katika hatari pia, msongo wa mawazo na matatizo ya kifamiliaNaye Isabela John anasema yeye alijifungua mtoto njiti akiwa na miezi saba  na kutokana na likizo kuwa ni siku 84 alilazimika kurejea kazini huku mtoto wake akiwa ndio kwanza anatimiza umri wa miezi tisa muda halisi mbao  ndio watoto wachanga kikawaida hupaswa kuzaliwa  na hapo ndio mama hutakiwa kuanza likizo mbao adi anamaliza siku 84 walau mtoto anakua anakaribia miezi mitatu tofauti na mtoto njiti ambaye atakua anatimiza miezi tisa na siku kadhaa na kuachwa

“’Sisi wanawake ambao tunajifungua watoto wa aina hii huku tukiwa kazini tukiongezewa muda wa likizo kutoka siku 84 za sasa tutaweza kutekeleza majukumu yetu kwa ufanisi kwenye malezi na kazini pindi tunaporejea kwa kuwa hakutakuwa na mawazo mengi kichwani ya kumuwazia mtoto huyu”’amesema Isabela.

Aidha Sikitu Salumu  mama aliyejifungua pia mtoto njiti katika hospitali ya Tumbi  Kibaha wakati wa kilele cha siku ya Wanawake Duniani anasema ni mara yake ya kwanza kujifungua mtoto wa  mieizi saba na kwamba mwanzo aliogopa hata kumuangalia mwanaye kutokana na kuwa ni mdogo mno machoni na pia hata uzito wake .

"Natoa wito kwa jamii kuna baadhi yao wamekuwa wakihusisha na imani potofu pindi mwanamke anapojifungua mtoto njiti jambo ambalo siyo kweli ni lazima watambue kuwa kila kitu kinapangwa na Mungu hivyo tunapaswa tuwapende watoto wanaozaliwa kabla ya wakati na si kuwawazia vibaya"amesema Sikitu ambaye ni mama wa watoto watatu na ni mara yake ya kwanza kujifungua mtoto njiti.

         

Hali ikoje

Kwa mujibu shirika la Umoja wa Mataifa la afya Duniani WHO na shirika la umoja wa mataifa la kuhudumia watoto UNICEF makadirio yanaonyesha kwamba mwaka 2020 takribani watoto milioni 13.4 walizaliwa kabla ya muda yaani njiti huku karibu milioni 1 kati yao wakifariki kutokana na matatizo yanayotokana na hali hiyo ya kuzaliwa kabla ya wakati .

Akizungumzia changamoto hiyo, Afisa elimu kazi wa chama cha wafanyakazi wa Serikali kuu na afya (TUGHE) makao makuu Nsubisi  Mwasandende amesema  sheria ya sasa ya  ajira na mahusiano kazini imekuwa ikitoa siku 84 kwa wanawake wanaojifungua mtoto mmoja na siku 100 kwa wanaojifungua zaidi ya mtoto mmoja .

Lakini sheria hiyo haisemi chochote kuhusu wale wanawake wanaojifungua watoto njiti  hivyo wanaikumbusha Serikali ifanyie kazi changamoto hiyo. 

"Sheria ya sasa ya  ajira na mahusiano kazini imekuwa ikitoa siku 84 kwa wanawake wanaojifungua mtoto mmoja na pia siku 100 kwa wanaojifungua zaidi ya mtoto mmoja  wala haisemi chochote kuhusu wanawake wanaojifungua watoto njiti ndio maana tumeona ni vyema kuikumbusha Serikali ili ifanye mabadiliko ili kuwaongezea muda wanawake hao"amesema  MwasandendeAfisa elimu kazi wa chama cha wafanyakazi wa serikali kuu na afya (TUGHE) makao makuu Nsubisi  Mwasandende

Awali. chama cha wafanyakazi wa Serikali kuu na afya Tanzania (TUGHE) Mkoani Pwani katika kuelekea kilele cha siku ya wanawake  wametoa vifaa mbalimbali vya usafi na vitenge katika wodi ya watoto njiti  Hospitali ya rufaa ya mkoa Tumbi 

Nini kauli ya Serikali Bungeni suala hili lilipoulizwa na Wabunge ?

 Akizungumza   Juni  25,2019  wakati wa kikoa cha Bunge jijini Dodoma aliyekuwa Naibu Waziri wa nchi ofisi ya Raisi Utumishi na utawala bora  Mary Mwanjelwa alisema kuwa Serikali  imeweka utaratibu kwa mtumishi wa umma anayejifungua pacha zaidi ya wawili au  watoto njiti.

Alisema kwamba  mwajiri wake anapaswa kuwailisha hoja kwa katibu Mkuu (Utumishi) Ili kupata kibali cha kuongezewa muda wa likizo.

"'Ikitokea mtumishi wa umma kajifungua watoto mapacha zaidi ya wawili au watoto njiti na kulazimika kuwa na muda zaidi wa kuhudumia watoto hao,mwajiri wake anapaswa kuwasiliana hoja kwa katibu Mkuu (Utumishi)Ili atoe kibali cha kuongezewa muda wa likizo ya uzazi"alisema (nukuu)

 Waziri huyo alikuwa akijibu maswali kutoka kwa wabunge pia alitoa wito kwa waajiri na wasimamizi wa rasilimali watu katika utumishi wa umma kutoa taarifa kwa katibu mkuu (Utumishi) kuomba kibali cha kuongezewa muda wa likizo ya uzazi kwa watumishi wa umma waliochini yao watakapojifungua watoto pacha zaidi ya wawili au watoto njiti.

Matatizo kadhaa yanayoweza kumkumba mtoto njiti

Matatizo yanayowakumba zaidi watoto njiti ni pamoja na kupumua kwa sababu wakati huu mapafu yanakua hayajakomaa, shida ingine mi kwenye ulaji au unywaji kutokana na mfumo change wa chakula

Katika kutilia msisitizo na kuonyesha umuhimu wa kuwajali wanawake wanaojifungua watoto njiti TUGHE makao makuu  Pwani wametembelea na kutoa misaada mbalimbali kwenye wodi ya wanawake waliojifungua watoto njiti katika hospitali ya rufaa mkoa wa Pwani Tumbi ikiwa ni sehemu pia ya maadhimisho ya siku ya wanawake mkoani humo sherehe zilizofanyika kimkoa kwenye viwanja vya Mlandizi halmashauri ya Wilaya ya Kibaha.Mwenyekiti wa idara ya wanawake (TUGHE) makao makuu Agnes Ngereza amesema wameona ni vema kuwatembelea na kutoa msaada vifaa vya usafi  na nguo za kusitiri  watoto wachanga na akina mama kwenye wodi ya wanawake waliojifungua watoto njiti  na pia lengo ni kupata changamoto mbalimbali zinazowakabili ili kuziwasilisha kwa wadau wengine ili kupata uvumbuzi.

 Kadhalika Muuguzi bingwa wa watoto Hospitali ya Tumbi Maua Pendo ameushukuru uongozi wa TUGHE kwa kutoa msaada huo kwa wanawake na kuziomba taasisi zingine kuiga mfano huo.









 Club News Editor

Comments

Popular posts from this blog

RC PWANI AONGOZA WAKAZI PWANI KUJIANDIKISHA KWENYE DAFTARI LA WAPIGA KURA

BARAZA LA MADIWANI KIBAHA MJINI LAMPONGEZA MKURUGENZI WAKE KWA KAZI NZURI ANAYOIFANYA SAMBAMBA NA KUONGEZA MAPATO.

RAIS SAMIA ATANGAZA KIBAHA MJINI KUWA MANISAPAA,MBUNGE KOKA AFURAHIA ASEMA KIBAHA ITANG'AA