MATOKEO YA SENSA 2022 NA MATUMIZI YAKE KWA MAENDELEO YA TAIFA, WANAHABARI WAJENGEWA UWEZO KUELIMISHA JAMII.


 

Na mwandishi wetu Pwani.

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ilifanya Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022. Baada ya  kukamilisha awamu mbili za kwanza za utekelezaji wa Sensa hiyo, Serikali imo katika awamu ya tatu na ya mwisho ya utekelezaji wa Sensa hiyo inayojumuisha uchakataji, uchambuzi, uandishi wa ripoti, usambazaji na mafunzo ya Matumizi ya Matokeo hayo ya Sensa ya Mwaka 2022.


Katika awamu ya tatu ya utekelezaji wa Sensa ya Watu na Makazi ya 2022 Wanahabari wa mikoa ya Pwani, Morogoro na Tanga wamejengewa uwezo namna ya kupata Matokeo, kuyatafsiri na kuyatumia katika kusambaza na Kuelimisha jamii kuhusu namna ya Matumizi yake. 


 Akifungua Mafunzo hayo yalifanyika kwa siku mbili tarehe 16 na 17 Jijini Tanga. Katika ufunguzi wa Mafunzo hayo Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga Ndugu Sebastian Masanja ameeleza umuhimu wa kazi za wanahabari katika jamii na Wananchi wanatambua kazi hizo. Alitoa Rai kwa wanahabari kwenda kuelimisha wananchi juu ya Matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022.


Mafunzo hayo yalitanguliwa kwa kueleza uwepo  Ofisi  ya Taifa ya Takwimu na majukumu yake na pia kujua aina tofauti za Takwimu zitolewazo na Ofisi ya Taifa ya Takwimu zinazochambuliwa Kiuchumi, Kijamii na Kimazingira.


Mafunzo hayo yalibeba uwezo wa  kuchambua Matokeo ya Sensa ya 2022 na kuweza kuyatafsiri kutafuta na kutatua Changamoto mbalimbali kwa maendeleo ya jamii.




Club News Editor - Charles Kusaga


Comments

Popular posts from this blog

RC PWANI AONGOZA WAKAZI PWANI KUJIANDIKISHA KWENYE DAFTARI LA WAPIGA KURA

BARAZA LA MADIWANI KIBAHA MJINI LAMPONGEZA MKURUGENZI WAKE KWA KAZI NZURI ANAYOIFANYA SAMBAMBA NA KUONGEZA MAPATO.

RAIS SAMIA ATANGAZA KIBAHA MJINI KUWA MANISAPAA,MBUNGE KOKA AFURAHIA ASEMA KIBAHA ITANG'AA