LIGI YA SOKA YA MABINGWA WA MIKOA YAANZA KWA MBWEMBWE PWANI



Na Gustafu Haule,Pwani

MASHINDANO ya Ligi ya Mabingwa wa Mikoa yameanza kutimua vumbi Machi 8, mwaka huu katika viwanja vya Tamco vilivyopo Mjini Kibaha kwa kuzikutanisha timu ya  Kiduli FC  na Black Six ya Jijini Dar es Salaam .

Katika mchezo huo Black Six wameibuka na ushindi wa bao 1-0  lililofungwa katika dakika 41 ya  kipindi cha kwanza kupitia mchezaji wao Kelvin madalisto aliyefunga kupitia mpira wa kichkiwa uliopigwa kutoka kulia mwa dimba hilo.

Kocha wa Kiduli FC Hery Kisanga , amesema kuwa mchezo wao wa kwanza wamefungwa kutokana na makosa yaliyofanywa na wachezaji wake lakini kufungwa kwao hakuwafanyi kukata tamaa .
Kocha wa Kiduli FC Hery Kisanga ,akizungumza  mara baada ya kumalizika kwa mchezo dhidi ya Black Six uliopigwa katika dimba la Tamco -Kibaha Machi 08 ,2024.

Kisanga, amesema kuwa kwasasa wanajipanga na michezo mingine inayofuata na watakwenda kuyafanyiakazi mapungufu yaliyojitokeza na ana imani michezo ijayo itakwenda kuzaa matunda.

"Leo tumefungua mashindano haya lakini tumekubali kupoteza mchezo huu lakini tunaenda kuyafanyiakazi mapungufu yaliyojitokeza na tunaimani tutafanya vizuri,"amesema Kisanga

Kisanga ,amewaomba washabiki wa Mkoa wa Pwani kujitokeza kwa wingi katika kuisapoti timu yao pale inapocheza ili hiweze kupata nguvu ya ushindi wa michezo mingine ijayo.

Kwa upande wake kocha wa Black Six Omary Mbweze ,amesema siri ya ushindi wao ni wachezaji wake kujituma na kutumia vizuri nafasi waliyopata huku akiongoza kuwa ushindi huo umewapa nguvu ya kupambana na michezo mingine ijayo.

Hatahivyo,kituo cha Mkoa wa Pwani  kimejumuisha timu zote zilizopangwa kundi B ikiwemo Singida Cluster,Black Six,Moro Kids,Stand FC,Red Angels,Gunners FC,na wenyeji Kiduli FC.
Kocha wa timu ya Black Six  Omary Mbweze akizungumza mara baada ya kumalizika kwa mchezo kati ya timu yake na Kiduli FC uliopigwa katika dimba la Tamco Kibaha Mjini.










Club News Editor Julieth Ngarabali

Comments

Popular posts from this blog

RC PWANI AONGOZA WAKAZI PWANI KUJIANDIKISHA KWENYE DAFTARI LA WAPIGA KURA

BARAZA LA MADIWANI KIBAHA MJINI LAMPONGEZA MKURUGENZI WAKE KWA KAZI NZURI ANAYOIFANYA SAMBAMBA NA KUONGEZA MAPATO.

RAIS SAMIA ATANGAZA KIBAHA MJINI KUWA MANISAPAA,MBUNGE KOKA AFURAHIA ASEMA KIBAHA ITANG'AA