KIKWETE AKABIDHI PIKIPIKI KWA MAAFISA UGANI CHALINZE
Julieth Ngarabali, Chalinze
Mbunge wa Jimbo la Chalinze Mkoani Pwani Ridhiwani Kikwtete amekabidhi pikipiki sita kwa Maafisa Ugani wa Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze ikiwa ni sehemu ya kuendelea kuwapatia Vitendea kazi Watumishi wa kada hiyo katika sekta ya Kilimo na Mifugo kwenye halmashairi hiyo.
Ikumbukwe kuwa Ridhiwani pia ni Naibu Waziri katika Ofisi ya Rais manejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala bora.
Amesema pikipiki hizo
zimetolewa na Serikali Kuu kupitia Wizara ya Kilimo na kwamba zinalenga kuwawezesha maafisa Ugani
kuweza kufika katika maeneo ya kwa wenye uhitaji ili kuwezesha kilimo bora.
Kugawiwa kwa pikipiki hizi kunafanya maafisa ugani waliopewa
vifaa hivyo kufika 14 kati ya kata 16 za Halmashauri hiyo.
Halmashauri ya Chalinze ni moja kati ya Halmashauri
zinazoongoza kwa kilimo katika eneo la
Mashariki ya Tanzania.
Comments
Post a Comment