HIVI NDIVYO KAMPENI YA UCHAGUZI CCM MSANGANI ILIVYOANZA KIBAHA


Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais ,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) Mohamed Mchengerwa akimnadi mgombea wa udiwani wa Kata ya Msangani kwa tiketi ya CCM Gunze Chongela katika ufunguzi wa kampeni uliofanyika jana katika viwanja vya juhudi vilivyopo kwenye Kata hiyo 

Na Gustafu Haule,Pwani

WAZIRI wa Nchi,Ofisi ya Rais ,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) Mohamed Mchengerwa,amesema Serikali ya awamu ya Sita imeweka mpango maalum wa kuhakikisha inajenga Shule za Sekondari na Msingi katika Kata ambazo hazina Shule.

Mchengerwa ambaye pia ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa( NEC) ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na wananchi,wanachama na viongozi wa Chama Cha Mapinduzi katika uzinduzi wa kampeni za udiwani Kata ya Msangani Halmashauri ya Kibaha Mjini zilizofanyika Machi 9 .

Amesema kuwa,Serikali ya awamu ya Sita chini ya Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan inatambua umuhimu wa elimu hapa nchini na kwamba kila siku inaendelea kuweka juhudi za kuimarisha miundombinu ya elimu kote nchini.

Mchengerwa amesema kwasasa Serikali imeweka mpango maalum wa kuendelea kujenga shule katika maeneo ambayo yanahitaji kuwa na shule na kwamba Shule zitakazojengwa ni zile za Msingi na Sekondari.
"Serikali inaendelea kuyafanyiakazi mapungufu yaliyopo katika elimu ikiwemo kujenga Shule katika maeneo yote yanayohitajika kuwa na shule kwani adhma ya Serikali ni kuhakikisha watoto wote wanaofikia umri wa kwenda shule wanapata fursa ya kusoma bila vikwazo,"amesema Mchengerwa.

Aidha,Mchengerwa amewataka Wana CCM kuzisemea kazi zilizofanywa na Rais Samia katika kipindi alichokaa madarakani ili Wananchi waweze kujua kazi za kimaendeleo zilizofanyika na hivyo kumpa Rais nguvu ya kufanya mazuri zaidi.

Kuhusu kampeni za udiwani Kata ya Msangani Mchengerwa amewataka Wananchi wa Kata hiyo kuhakikisha wanamchagua mgombea wa CCM Gunze Chongela  kwakuwa ndio chama pekee kinachoweza kuwaletea maendeleo.

Amesema,wakichagua chama kingine watakuwa wamejiharibia kwakuwa wanaweza kuchelewesha maendeleo katika Kata yake kwani CCM ili iweze kufanyakazi vizuri inahitaji diwani wa CCM,Mbunge wa CCM na Rais kutoka CCM.

Kwa upande wake mgombea wa udiwani Kata ya Msangani kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Gunze Chongela amesema kuwa anatambua changamoto zilizopo katika Kata hiyo na kwamba wakimchagua changamoto zote zitakuwa zimepata ufumbuzi.
Mgombea wa udiwani Kata ya Msangani kwa tiketi ya CCM Gunze Chongela (Kulia)akiomba kura kwa Wananchi katika ufunguzi wa kampeni uliofanyika jana katika viwanja vya juhudi vilivyopo katika Kata hiyo.

"Mimi ni mkazi wa hapa natambua changamoto za Kata yangu ya Msangani kwahiyo nikopesheni imani yenu kwa kunipa kura za ndio nami nitawalipa maendeleo,"amesema Chongela.

Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kibaha Mjini Mwajuma Nyamka, amesema kuwa CCM ni chama imara na kinatakiwa kushinda katika uchaguzi huo ili kukipa urahisi chama wa kufanya maendeleo .

Nyamka,amewaomba Wananchi wa Kata hiyo kuungana kwa pamoja kumchagua mgombea wa CCM Gunze Chongela kuwa diwani wa Kata ya Msangani ili aende kuwasemea changamoto zao katika Baraza la madiwani la Halmashauri ya Mji Kibaha .










Club News Editor, Julieth Ngarabali

Comments

Popular posts from this blog

RC PWANI AONGOZA WAKAZI PWANI KUJIANDIKISHA KWENYE DAFTARI LA WAPIGA KURA

BARAZA LA MADIWANI KIBAHA MJINI LAMPONGEZA MKURUGENZI WAKE KWA KAZI NZURI ANAYOIFANYA SAMBAMBA NA KUONGEZA MAPATO.

RAIS SAMIA ATANGAZA KIBAHA MJINI KUWA MANISAPAA,MBUNGE KOKA AFURAHIA ASEMA KIBAHA ITANG'AA